Baadhi ya mili ya watu waliozama kwenye meli ya abiria na mizigo ya Spice iliyokuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba imeanza kuletwa nchi kavu katika bandari ya Nungwi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye eneo la tukio vikosi vya ukozi vya KMKM pamoja na vyombo vingine vya wananchi vinaendelea na shughuli za ukozi.
Akizungumza na vyombo vya habari naibu waziri wa miundo mbinu na mawasiliano Issa Haji Gavu amesema vyombo vya uokozi vimeondoka bandari ya Malindi kuelekea katika eneo la tukio.
Gavu amesema msiba huo ni wa kitaifa na kuwataka wananchi kuendelea kuvuta subra na serikali itatoa taarifa rasmi juu ya maafa hayo.
Hata hivyo idadi ya watu waliokuwemo ndani ya meli hiyo na walionusurika bado haijafahamika, lakini baadhi ya viongozi wa serikali waliozungumza na vyombo vya habari wamesema watu kadhaa wamefariki dunia.
Meli hiyo ya Spice imezama usiku wa manane katika mkondo wa Nungwi na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
Wananchi wa Tanzania wameingiwa na simazi kutokana na kuguswa na msiba huo
Taarifa za hivi karibuni zinasema meli hiyo inaendelea kukokowata na maji na mawimbi ya bahari ikielekea katika mkoa wa Tanga
NEW NEW NEW
Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebiruka na kuzama katika Bahari ya Hindi katika Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.
Naibu Waziri huyo amesema meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima,lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.
Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unahitajika.Jeshi la Polisi Tanzania imetuma Helkopta yake kwenye eneo la tukio.
Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.
Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.
TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR KUHUSU AJALI YA MELI
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ametoa salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa kufuatia ajali ya meli ya Spice Islander na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia.
Akizungumza katika eneo la kupokelea majeruhi na maiti wa ajali hiyo huko Nungwi amesema msiba huo ni mkubwa na umegusa taifa na wananchi wote wa Zanzibar.
Hivyo amewataka ndugu, jamaa na wananchi kwa ujumla kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki cha msiba.
Dr. Shein amesema serikali imeandaa utaratibu wa kuwahudumia waliokufikwa na maafa hayo na wale waliopoteza maisha, serikali itafanikisha mazishi yao.
Hata hivyo Dr. Shein amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi waliochukua hatua za awali za kuokoa maisha ya watu.
Aidha Dr. Shein amevitaka vyombo vya habari kutoa habari zenye usahihi ili kuwasaidia wananchi kupata taarifa za maafa hayo kwa usahihi.
Taarifa za hivi karibuni meli hiyo iliyokuwa na zaidi ya watu 610 hadi sasa watu 260 wameokolewa wakiwa hai.

14 responses to “AJALI YA MELI YATOKEA ZANZIBAR, WATU KADHAA WAFARIKI DUNIA, JUHUDI ZA UKOZI ZINAENDELEA”
Hassan Said
September 10th, 2011 at 08:51
Poleni wafiwa wote na mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.Hili liwe fundisho kwa vyombo husika vya usalama majini hasa Sumatra
Jackline
September 12th, 2011 at 07:10
Poleni watanzania wenzangu,2kumbuke mungu alitwaa,na wala 2sianze kulahumiana.
frank obed lungwa
September 12th, 2011 at 19:21
ni kipindi kigumu kwa taifa letu.tuache kutafuta wa kumlaumu kwa sasa kwani tatizo limeshatokea cha muhimu watanzania tudhihirishe ukarimu wetu kwa kujitolea kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli.mwenyezi mungu atujaalie moyo wa subira ili tuvuke salama katika kipindi hiki kigumu.
mungu ibariki tanzania,mungu ibariki zanzibar.
SALEH MREH
September 13th, 2011 at 06:50
POLENI WAFIWA WOTE. MSIBA WETU SOTE!
mohamed mtumwa hamad
September 13th, 2011 at 09:36
Polen wafiwa wote kwani hiyo ni kazi yake MWENYEZI MUNGU kwa Allah asema nitakuleteen kila mtihan kwa hiyo na huo ni mtihani wake .
frank obed lungwa
September 13th, 2011 at 17:54
siku zote mamlaka zilizopewa dhamana ya kuongoza sekta mbalimbali hujisahau na hukumbuka majukumu yao wakati tayari athari kubwa zimeshatokea.tusilaumiane ila tuwachangie waathirika na iwe fundisho kwa wenye dhamana.
frank obed lungwa
September 13th, 2011 at 18:30
MAMLAKA ZILISAHAU AJALI YA MV BUKOBA ILISABABISHWA NA NINI NDIO MAANA MAKOSA YALEYALE YAMEJIRUDIA.TAMAA ZA WATU WACHACHE ZINAANGAMIZA MAISHA YA WATANZANIA.
FREDRICK ERNEST MGONGOLWA
September 14th, 2011 at 05:18
poleni watanzania wote kwa msiba uliotokea.
hii inaonyesha hakuna uwajibikaji inchini kwetu.kitengo cha usafiri cha nchi kavu,anga na maji hakifuatilii ubora wa vyombo ndiyo maana ajali nyingi zinatokea kila kukicha.
mfano basi linatoka Dar-mwanza kila siku kwenda na kurudi ni saa ngapi linakaguliwa kama breki,cluch na viungo vingine vya mabasi hayo vipo salama kwa safari achilia mbali ubora wa matairi.
Idara hii ipo tu kwa ajili ya maslahi binafsi bila kujali ni jinsi gani wananchi walipa kodi wanaowafanya waende kazini na familia zao kuishi vizuri wanapata tabu na usumbufu mkubwa.
mungu awerehemu marehemu wote
ameen.
mungu aiweke mioyo ya marehemu wote mahali pema peponi .
Kassim
September 21st, 2011 at 03:04
Mamlaka husika ziwajibishwe. Kwa uzembe ulio jitokeze.
Aliy masoud
November 25th, 2011 at 18:25
Hakika siku hii hatutoisahau katika maisha yetu ee mwenyezi mungu waweke pema pepo waja wako wote waliotutoka katika msiba huu aamin…
Denis Ande
December 30th, 2011 at 11:39
hmjambo jambo huko bana
frank obed lungwa
January 21st, 2012 at 20:14
mi ni mkristo lakini siku zote nina ndoto za kufanya kazi ya ngu hii ya ualimu mjini zanzibar.shule yoyote ilyo tayari kuniajiri(msingi)iwasiliane nami kwa simu namba 0685123891 mi nipo mkoa wa mara.
frank obed lungwa
January 21st, 2012 at 20:22
kwa mwalimu yoyote wa shule ya msingi katika mkoa wa dodoma au morogoro anayetaka kubadilishana nami kituo cha kazi mkoa wa mara_serengeti awasiliane nami kwa simu namba 0685123891
wgagkj
March 23rd, 2012 at 21:03
jehis