Archive for September, 2009

ZANZIBAR ISLAMIC NEWS BLOGI KWA HABARI ZA KITAIFA, MAKALA ZA KISLAMU, NAFASI ZA MASOMO, KAZI, N.K

ZANZIBAR ISLAMIC NEWS NI BLOGI ILIYOANDALIWA NA MWANDISHI WA HABARI JUMA ABDALA ALI

Advertisements

Kumalizika kwa Mwezi wa Ramadhan isiwe mwisho wa Ibada

Enyi Mlioamini!m melazimishwa kufunga (Saumu)kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu”(2:183)

 

Na Ramadhan Himid, Zanzibar.

 

WAISLAMU hivi sasa wapo katika heka heka za kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini la muhimu ambalo waislamu hao wanatakiwa kulikumbuka ni ule utii wa hali ya juu kwa Mola wao waliouonyesha wakati wa mwezi huo mtukufu.

  Kwa maana hiyo Mungu yule yule aliekuwa akiheshimiwa kwa utii mkubwa ndani ya Ramadhan, bado yupo milele na milele hivyo wakati wote anahitaji kuheshimiwa kwa kufuata yale aliyoyaamrisha na kuacha yale aliyoyakataza.

  Mwezi huo mtukufu ulikuwa ni darasa tosha kwa baadhi ya dada zetu wanaopenda kuvaa nguo zisizoendana na maagizo ya Dini ya Kiislamu na hivyo yale mabaibui waliyokuwa wakiyavaa wakati wa mfungo wa Ramadhan , waendelee na tabia hiyo kwa kuwa Mungu aliyekuwepo wakati wa Ramadhan ndiye yule yule aliyeko milele .

  Wanawake wenye tabia kama hiyo ya kuvaa watakavyo wasijidanganye kwamba Mungu wa Ramadhan hatamani kuona miili yao, na hivyo kumalizika kwa Ramadhan waachwe wafanye tu watakavyo.

   Tusimchezee Mungu kwani mwanamke akionekana unyoya mmoja tu wa nywele zake na mtu ambaye si maharimu wake, kwa maana mumewe au jamaa zake kama baba yake au mama yake siku ya Kiyama atavutwa nywele zake hadi kwenye mashimo ya moto, sasa seuze kila siku kutembea uchi.

   Kwa kweli dada zetu ndani ya Ramadhan walikuwa wakipendeza kwa kuvaa mavazi ya heshima kiasi kwamba vile vishawishi vya zinaa vilikuwa sitrahisi kuchemka mwilini mwa mwanamume.Subiri Ramadhan imalize utawaona kama wanagombea umisi kila mmoja anamshinda mwenzake kwa kuvaa uchi.Lahaulah.

   Basi bila shaka tumeshuhudia wenyewe kwa jinsi imani zetu zilivyonawirika ndani ya mfungo wa Ramadhan.Waliokuwa hawasali miezi mengine yote waliacha uvivu wao wakajitakasa kwa Mola wao.

   Kama vile haitoshi Wengi tulikuwa tukikesha usiku kucha kusali Sala za usiku kama Tahajud, Sunna za Haja, Witri na kadhalika pamoja na kuleta kila aina ya maghafira kiasi kwamba mioyo yetu wakati alipokuwa akitajwa Mola wetu Allah (S.W) na Mtume wake Muhammad (S.A.W) ilijawa na hofu kubwa kuashiria kuwa kweli tuliiva kiimani.

   Tupo pia tuliolia usiku kucha kutubia madhambi yetu tuliyoyafanya, na Mungu atulipe shufaa njema kutokana na nia zetu, lakini tukumbuke kuwa mwisho wa Ramadhan sio mwisho wa Ibada.

  Si hivyo tu bali wapo pia wale waliojaliwa kukaa itikafu misikitini kwa kipindi cha kumi zima la mwisho wa mfungo wa Ramadhan huku wakimhimidi Mola wao pamoja na kumtaka msamaha mwema hapa duniani na kesho Akhera.

   Mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1430 AH ndio unaelekea ukingoni, kama wasemavyo maulama na wahadhiri mbali mbali wa dini hii ya Kiislamu kwamba jambo la muhimu kwetu kabla ya kusherehekea Sikukuu ya Idd-el-Fitr ni kujitathmini kwa kiasi gani tunaweza kuendeleza yale mafunzo mema tuliyoyapata ndani ya Ramadhan?

       Na hapa ndipo panapo tatizo, maana hata ukianza kufanya tathmini ndogo Misikitini utagundua kuwa hata wale waliokuwa wakisali kwa wingi kipindi hiki cha Ramadhan idadi inaanza kupungua mwishoni mwa kumi hili la mwisho muhimu la kuachwa huru na moto.

  Kwa kweli inasikitisha kuona kuwa baadhi yetu tumeanza kupungua Misikitini kama kwamba Mungu wa Ramadhan ndio anaondoka na hivyo tutaonana nae tena mwaka akipenda Inshaallah.

   Tumesahau ile hadithi ya Mtume (S.A.W) isemayo kwamba ‘Mcheni Mwenyezi Mungu popote mulipo na ishini na watu kwa wema, na jitakaseni kwa wema punde tu munapoteleza kwenye maovu”.

  Katika hadithi hiyo ya Mtume (S.A.W) anatilia mkazo juu ya kumcha Mungu pahala popote ama mazingira yeyote mtu aliyopo bila kujali kuwa huu ni mfungo wa Ramadhan au huu ni mwezi wa kula mchana.

  Kwa kumuabudu Mungu mwezi mtukufu wa Ramadhan tu pekee tusitegemee hata siku moja kuwa Mungu wetu atatuepusha na Moto wa Jehannam.

  Wako wapi wale waislamu waliorehemewa na Mola wao kumi la mwanzo wa mwezi wa Ramadhan, wako wapi pia wale waislamu waliofutiwa madhambi yao katika kumi la pili la Ramadhan na je wako wapi wale walioachwa huru na moto. Hawapo tena Ramadhan imekwisha na hivyo wanafunga virago vyao vya kambi ya Ramadhan hadi mwakani.

  Lakini je ni nani kati yetu ana uhakika kuwa atafika Ramadhan ijayo mwaka 1431AH, basi tusihadaiwe na pumzi tunazovuta bila ya kulipia bili. Tusimuasi Mungu kwa makusudi tukidhani kuwa tunamtogoza wakati yeye akisema kuwa basi fayakun.

   Wale waliokula mchana wa mwezi wa Ramadhan kwa kujificha mbele ya kadamu nasi wakajiona wajanja waliorevuka, wajue tu kwamba hawakuwaonea haya binadamu wenziwao bali pia hawakumuonea haya Mungu wao ambaye anaona kila kitu kinachotendeka katika ulimwengu huu.

  Waislamu wa namna hiyo waliojitoa mshipa wa fahamu kwa kutoa kila aina ya visingizio ili wasifunge na wajiulize wamezidi nini , ndio wamenenepa kwa kula sana mchana kutwa au ni hasara tu kwa Mola wao kesho Akhera?,Bila shaka hawana walichokivuna ila hasara ya Jahanam.

   Hivyo ni vyema kukumbushana juu ya jambo hili kuwa kumalizika kwa mwezi wa Ramadhan si mwisho wa Ibada, kwani Ibada inaendelea kila siku tokea mtu anapoamka mpaka anapolala.

   Tumuombe Mwenyezi Mungu atutakabalie funga zetu na atuzidishie imani juu ya kuendeleza mafunzo mema tuliyoyapata katika mwezi huo mtukufu.

10 MBARONI KWA FUJO ZA UANDIKISHAJI KASKAZINI ‘A’

Na Juma Abdallah Ali

Zenji fm

MKOA WA KASKAZINI UNGUJA:

        Zaidi ya watu kumi wakiwemo wanawake wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusishwa na ghasia za uandikishaji zilizotekea katika vituo vya uandikishaji vya dafatari la wapiga kura wilaya ya Kaskazini “A”.

        Watu hao wamekamatwa katika vituo vya Nungwi, Potoa, Fukuchani na Kidoti kwa madai ya kufanya ghasia baada ya kukataliwa kuandikishwa kutokana na kukosa vitambulizho vya ukaazi.

        Hata hivyo baadhi ya vituo vya unadikishaji huo vilikuwa na utulivu, lakini idadi ya wanaoandikishwa ilikuwa ndogo.

        Mwandishi wetu alietembelea katika vutuo vya uandikishaji vya wilaya ya kaskazini “A” amesema wengi waliokuja kujindikisha wamechukua barua za masheha badala ya vitambulisho vya ukaazi.

 

                                        …..2…MKOA WA KASKAZINI UNGUJA…

MKOA WA KASKAZINI UNGUJA…….2

 

        Akizungumza na Zenji Fm Radio katika vituo vya uandikishaji vya Fukuchani, Nungwi, Kendwa, Muwange, Kidoti, Potoa na Bwereu baadhi ya wananchi wamesema wamekosehwa vitambulisho hivyo licha ya kuwa na barua za sheha……CLIPS……(SAVED-UANDIKISHWAJI)

        Nao baadhi ya masheha wakizungumzia suala hilo wamesema wao wametimiza wajibu wao wa kuwapa wananchi barua za kupatiwa vitambulisho………CLIPS…..(SAVED-MASHEHA)

 

UANDIKISHAJI WA WAPIGA KURA WADORORO KASKAZINI ‘A’

Na Juma Abdalla Ali

Zenji Fm

WILAYA YA KASKAZINI ‘A’:

        Kazi za uandikishaji wa dafatari la wapiga katika wilaya ya Kaskazini “A” zimeonekana kudhorota kutokana na wananchi wengi kukosa vitambulisho vya ukaazi.

        Mwandishi wetu alietembelea vituo hivyo amesema wananchi wameitikia wito wa kutaka kuandikishwa kama wapiga kura, lakini wengi wao hawana sifa ikiwemo kukosa kitambulishi hicho na badala yake kuwa na barua za sheha.

        Wakizungumza na waandishi wa habari wasimamizi wa vituo vya uandikishaji vya wilaya hiyo wamesema kazi hizo zimekuwa zikidhorota kutokana na idadi ndogo ya wanaojiandikisha…..CLIPS….(SAVED-WASIMAMIZI)

        Nae Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyi Chande amesema suala la wananchi kukosa vitambulisho vya ukaazi havihusiani na tume yake.

        Amesema tume hiyo imepeleka vifaa vya kutosha ili kuona kazi za uandikishaji zinakwenda vizuri na vituo vitaendela kuwa wazi hadi pale muda wake wa kufungwa utakapomalizika.                 15

WAHAMASISHENI VIJANA KUPATA VITAMBULISHO-KARUME

From Ikulu Zanzibar

PEMBA:           

        Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wazee kisiwani Pemba kuwahimiza vijana wao kuwa na vitambuisho vya ukaazi ili kuandikishwa katika daftari wapiga kura.

        Rais Karume amesema mwananchi yeyote aliyekuwa bado hajapata kitamblisho cha ukaazi afuate taratibu ili kupatiwa kitambulisho hicho na hatimae kuandikishwa kama mpiga kura.

        Hata hivyo rais Karume amesema kutokana na takwimu zinazotolewa na Idara ya Vitambulisho wananchi wengi wanavyo vitambulisho na hakuna sababu ya Daftari kutoendelea kuimarishwa.

        Akizungumza na wazee wa CCM kisiwani Pemba amesema lengo la kuwepo vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ni kuondoa manung’uniko na visingizio vinavyotokea wakati uchaguzi unapokaribia.

 

                                        …..2…PEMBA…..

 

 

PEMBA…….2

 

 

        Nao wazee hao wananchi walio wengi kisiwani humo tayari wanavyo vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.

        Wakizungumza na rais Karume kwa nyakati tofauti wakati wa ziara kisiwani Pemba wazee hao walimueleza Rais Karume kuwa wanaodai hawajapatiwa vitambulisho vya ukaazi maneno hayo si ya kweli na wana ajenda za siri.

        Nae mwakilishi wa jimbo la Tumbe Ali Bakar akizungumza na Zenji Fm Radio ameishauri serikali kuongeza kasi ya utowaji wa vitambulisho vya ukaazi ili watu wote wenye sifa waweze kuandikshwa katika daftari hilo…….CLIPS….(SAVED-BAKAR)

 

 

POLISI WATAKIWA KUTOJIINGIZA KWENYE SIASA-WAWAKILISHI

ZANZIBAR:                                      na Juma Abdalla

                                                        Zenj fm

        Jeshi la polisi la Zanzibar limetakiwa kutojiingiza katika masuala ya kisiasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwani linaweza kupoteza imani kwa wananchi.

        Wito huo umetolewa na kamati ya wajumbe wa baraza la wawakilishi ya katiba, sheria na utawala bora wakati ilipofanya ziara yake katika makao makuu ya jeshi hilo Kilimani mjini Zanzibar.

        Wajumbe hao wamesema endapo jeshi hilo halitakuwa imara linaweza kutumiwa vibaya na wanasiasa kutokana na utashi wao wa kisiasa wenye maslahi yao zaidi ya kibinafsi.

        Hata hivyo wajumbe hao wamelipongeza jeshi la polisi Zanzbar kwa jinsi inavyotekeleza majukumu yake ya kulinda na kusimamia maisha ya wananchi na mali zao licha ya kukabiliwa na uhaba wa vifaa.

        Nae kamishna wa polisi Zanzibar Khamis Simba amesema jeshi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya uhalifu kutokana na kutekelezwa sera ya polisi jamii ya ulinzi shirikishi.

VIONGOZI WA CCM, CUF WATOFAUTIANA KUREJEWA UANDIKISHAJI PEMBA

PEMBA

        Tume ya uchaguzi Zanzbiar kesho inatarajiwa kuanza tena kazi za uandikishaji wa daftari la wapiga kura katika mikoa ya Kaskazini Pemba na kaskazini Unguja, huku viongozi wa vyama vya CCM na CUF wakitofautiana juu ya uandikishaji huo.

        Akizungumza na zenji fm Radio kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid amesema bado watu kadhaa hawajapata vitambulisho vya ukaazi ili kuweza kuandikishwa katika dafrtari hilo.

        Amesema hali hiyo inaweza kuleta usumbufu kwa wananchi katika kupatiwa haki zao za kidemokrasia za kuwachagua viongozi wanaowataka……CLIPS…..(SAVED-UANDIKISHAJI)

         Nae naibu katibu mkuu wa CCM Saleh Ramadhan Ferouz ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika uandikishaji wa daftari hilo.

        Akitoa taarifa ya uandikishaji huko afisi kuu ya CCM Kisiwandui amesema kasoro zilizojitokeza katika uandikishwaji wa mwanzo zimeshapatiwa ufumbuzi, hivyo ni vyema kwa wananchi kuitumia nafasi hiyo ya kidemokrasia.

        Kazi za uandikishaji wa wapiga kura kisiwani Pemba ziliakhirishwa kiasi ya mwezi mmoja uliopita katika jimbo la Ole baada ya wananchi kutoingia katika vituo vya kujiandikisha.