Archive for January, 2010

BADILISHENI KATIBA TULINDE MARIDHIANO-SEIF

Na Juma Abdala Ali-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Chama cha wananchi CUF kimetoa wito wa kubadilishwa katiba ya Zanzibar ili kusogeza mbele uchaguzi mkuu na kutoa fursa kwa rais Karume kutekeleza maridhiano yaliofikiwa kati ya chama hicho.

Katibu mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad amesema kuahirishwa kwa uchaguzi huo sio kuongeza kipindi cha urais, lakini kutatoa fursa kwa rais Karume na yeye binafsi kutekeleza maridhiano hayo.

Akizungumza mara baada ya kupokea maandamano ya wananchi katika uwanja wa Kibanda maiti amesema licha ya rais Karume kutotaka kuongeza muda wa uongozi, amesema kwa hilo hana hiari kwa kile alichodai ni matakwa ya wazanzibari….CLIPS…..(SAVED-HAMAD)

Aidha bw. Hamad amewashauri wajumbe wa baraza la wawakilishi kubadilisha katiba ya Zanzibar ili kuchelewesha uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu ili kutoa nafasi ya kulea maridhiano hayo yaliofikiwa.

…….2..CUF…….

CUF…….2…..

Hata hivyo katibu mkuu huyo ametahadhirisha baadhi ya viongozi wanaojaribu kuviza maridhiano na kusema maridhiano hayo sio ya rais Karume wala Seif Sharif bali ni ya wazanzibari wote.

Hivyo amewataka viongozi wa serikali ya muungano kuelewa uzito wa suala hilo kwa vile Zanzibar ndio yenye matatizo na kuchelewesha uchaguzi huo sio jambo geni kwa Tanzania kwa vile limeshawahi kutokea mwaka 2005….CLIPS….(SAVED-BARA)

CUF YALAUMIWA KWA UKIMYA WAKE JUU YA TATIZO LA UMEME

NA JUMA ABDALA ALI-ZENJI FM

ZANZIBAR: Chama cha wananchi CUF kimetupiwa lawama kutokana na ukimya wake tokea kukatika kwa huduma ya umeme Disemba 10 mwaka jana na kuleta usumbufu kwa wananchi. Jumuiya ya kislamu ya Hiz-Ut-Tahrir ya Afrika ya mashariki, tawi la Zanzibar imesema CUF ndio chama kikuu cha upinzani kilitarajiwa kuikosowa serikali juu ya tatizo hilo, lakini kimekaa kimya. Taarifa ya jumuiya hiyo iliyotiwa saini na naibu katibu mkuu wake Sheikh Masoud Msellem imesema tatizo hilo lilipotokea mwaka 2008 chama cha CUF kilikuwa mkosowaji mkubwa, lakini hivi sasa kimekaa kimya huku bei ya chakula na bidhaa nyingine zikiongezeka kutokana na tatizo hilo. Aidha taarifa hiyo imesema tatizo la umeme katika kisiwa cha Unguja sio ukosefu wa raslimali, uchakavu wa mitambo au ukosefu wa utaalamu bali ni mfumo unaohitaji marekebisho. Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja limesababisha usumbufu kwa wananchi ikiwemo uhaba wa maji safi na salama pamoja na kuathiri kwa shughuli zao za uchumi. 16

KARUME ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA

NA JUMA ABDALA ALI-ZENJI FM

ZANZIBAR:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume ametoa msamaha kwa wafungwa 39 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Msamaha huo umewahusisha wafungwa wazee wenye maradhi, waliobakisha muda mfupi kumaliza kifungo chao, wanaofuata maadili mazuri, wafungwa wasioweza kufanya kazi kutokana na ugonjwa .

Hata hivyo msamaha huo hauwahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa makubwa yakiwemo biashara ya dawa za kulevya, wizi wa kutumia silaha, ubakaji na waliofungwa maisha.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar katika kifungu cha 59 kinampa uwezo rais kutoa msamaha kwa mfungwa yeyote alioko gerezani kuwa huru au kupunguziwa adhabu.

12

NIKO TAYARI KUUNGA MKONO SERIKALI YA MSETO IWAPO ITAKUWA NA MASLAHI NA ZANZIBAR-NAHODA

Na Juma Abdala Ali-Zenji Fm radio

ZANZIBAR:

Waziri kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha amesema iwapo chama cha Mapinduzi CCM kitakubali kuunda serikali ya mseto na chama cha wananchi CUF kwa ajili ya maslahi ya Zanzibar hatapinga mpango huo.

Amesema ana amini sera za CCM zinahimiza amani, umoja, mshikamano na maendeleo ya taifa, hivyo iwapo chama hicho kitafikia uwamuzi wa kuunda serikali hiyo ili wazanzibari washirikiane zaidi ataunga mkono mpango huo.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri kiongozi Nahodha amesema suala hilo bado halijafikishwa katika vikao vya chama, lakini endapo litafikishwa atatoa maoni hayo yenye maslahi na Zanzibari……..CLIPS…(SAVED-NAHODHA)

Akizungumzia mchango wa fedha wa serikali ya Jamahuri ya muungano juu ya tatizo la umeme amesema afisi yake imeshamuandikia waziri mkuu juu ya suala hilo na liko kwenye meza yake……CLIPS…(SAVED-KUOMBA)

Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja ilikatika tokea Desemba 10 mwaka jana na kusababisha usumbufu kwa wananchi ikiwemo uhaba wa maji na kuathirika shughuli zao za kiuchumi.   

16

KARUME ATEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI WA CCM KWA ASILIMIA 90

Na Juma Abdala Ali-Zenji Fm

ZANZIBAR;

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema imeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni tatu mwaka 2001 hadi shilingi bilioni 10 kwa mwezi mwaka 2009.

Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema hali hiyo imeiwezesha serikali kuwa na uwezo wake wa ndani wa kulipa mishahara ya watumishi wake na mafao ya wastaafu.

Akitoa tathmini ya uongozi wa rais Karume tokea kuingia madarakani mwaka 2000 kwa waandishi wa habari amesema benki ya watu wa Zanzibar imeimarishwa na kuongezeka amana za wateja kutoka shilingi bilioni 24 mwaka 2001 hadi bilioni 111 mwaka 2009.

Waziri kiongozi amesema hali hiyo imeifanya benki hiyo kuendeshwa kwa faida ya shilingi bilioni 4.5 kwa mwaka na kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali ambao wamekopeshwa zaidi ya shilingi bilioni 30.

Amesema serikali ya rais Karume imeimarisha miundo mbinu ya kiuchumi ikiwemo matengenezo ya bandari ya Malindi na kuiwezesha kufunga meli kubwa za mizigo kutoka mataifa mbali mbali.

…..2….ZANZIBAR……

ZANZIBAR……2..

Amesema kwa upande uwanja wa ndege umepanuliwa kutoka mita elfu mbili, 462 hadi mita elfu tatu na 22 na kuwezesha kutoa huduma kwa mashirika ya kimataifa yakiwemo Ethiopia, Comoro, Ujerumani, Uhispania, Itali, Kenya na Afrika ya kusini.

Waziri kiongozi ameyataja maeneo mengine yaliopiga hatua ni sekta ya elimu, afya, usambazaji wa umeme mijini na vijijini, maji safi na salama pamoja kuongeza wataalamu wazalendo.

Rais Karume anaetarajiwa kuondoka madarakani miezi tisa baada ya kufanyika uchaguzi wa mwaka 2010 serikali yake inadaiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia 90.

CHADEMA YATAKA KUSITISHWA MATUMIZI YA FEDHA ZA SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MIAKA 46

Na Juma Abdala Ali-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, kimepinga kuendelea kwa sherehe za Mapinduzi ambazo zitatumia mamilioni ya fedha huku wananchi wakikosa huduma ya umeme.

Akizungumza na Zenji Fm radio Naibu katibu mkuu wa CHADEMA Zanzibar Hamad Musa amedai zaidi ya shilingi bilioni tatu zitakazotumiwa katika sherehe hizo ni vyema zikaelekezwa katika kulipatia ufumbuzi tatizo la umeme.

Amesema hivi sasa tatizo hilo lililodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa limeharibu miundo mbinu ya kiuchumi na kijamii na kusababisha ukosefu wa huduma ya maji safi na salama.…….CLIPS…….(SAVED-CHADEMA)

Sherehe za mapinduzi Zanzibar ya miaka 46 ambazo kilele chake kitafikia Januri 12 Kisiwani Pemba hivi sasa zinaendelea kwa uzinduzi na ufunguaji wa miradi ya maendeleo na kiuchumi.

13

TANZANIA KUIMARISHA ULINZI KWENYE VIWANJA VYA NDEGE KUTOKANA NA TISHIO LA UGAIDI

DAR ES SALAAM:

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Laurent Masha amesema Tanzania imeimarisha ulinzi katika maeno yote ya viwanja vya ndege kufuatia kitendo cha raia mmoja wa Nigeria kutaka kuripua ndege moja ya Marekani nchini Uholanzi.

Kija huyo wa Nigeria Omar Farouk alikamatwa mwishoni mwa wiki wakati akijaribu kuripua ndege ya North West Aira Lines iliyokuwa iksafiri kutoka Ohalanzi kwenda Marekani.

Tukio hilo limesababisha viwanja vya ndege vya nchi mbali mbali kuimarisha upekuzi wa abiria hatua ambayo serikali ya Tanzania nayo imechukua hatua hiyo.

Tayari Marekani imemfungulia mashataka kijana huyo, huku rais Obama akitangaza kufanya tathimini mpya juu majeshi yake kukabiliana na vitisho vipya vya ugaidi.

13