Na Juma Abdala Ali-Zenji Fm

ZANZIBAR;

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema imeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni tatu mwaka 2001 hadi shilingi bilioni 10 kwa mwezi mwaka 2009.

Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema hali hiyo imeiwezesha serikali kuwa na uwezo wake wa ndani wa kulipa mishahara ya watumishi wake na mafao ya wastaafu.

Akitoa tathmini ya uongozi wa rais Karume tokea kuingia madarakani mwaka 2000 kwa waandishi wa habari amesema benki ya watu wa Zanzibar imeimarishwa na kuongezeka amana za wateja kutoka shilingi bilioni 24 mwaka 2001 hadi bilioni 111 mwaka 2009.

Waziri kiongozi amesema hali hiyo imeifanya benki hiyo kuendeshwa kwa faida ya shilingi bilioni 4.5 kwa mwaka na kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali ambao wamekopeshwa zaidi ya shilingi bilioni 30.

Amesema serikali ya rais Karume imeimarisha miundo mbinu ya kiuchumi ikiwemo matengenezo ya bandari ya Malindi na kuiwezesha kufunga meli kubwa za mizigo kutoka mataifa mbali mbali.

…..2….ZANZIBAR……

ZANZIBAR……2..

Amesema kwa upande uwanja wa ndege umepanuliwa kutoka mita elfu mbili, 462 hadi mita elfu tatu na 22 na kuwezesha kutoa huduma kwa mashirika ya kimataifa yakiwemo Ethiopia, Comoro, Ujerumani, Uhispania, Itali, Kenya na Afrika ya kusini.

Waziri kiongozi ameyataja maeneo mengine yaliopiga hatua ni sekta ya elimu, afya, usambazaji wa umeme mijini na vijijini, maji safi na salama pamoja kuongeza wataalamu wazalendo.

Rais Karume anaetarajiwa kuondoka madarakani miezi tisa baada ya kufanyika uchaguzi wa mwaka 2010 serikali yake inadaiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia 90.

Advertisements