NA JUMA ABDALA ALI-ZENJI FM

ZANZIBAR: Chama cha wananchi CUF kimetupiwa lawama kutokana na ukimya wake tokea kukatika kwa huduma ya umeme Disemba 10 mwaka jana na kuleta usumbufu kwa wananchi. Jumuiya ya kislamu ya Hiz-Ut-Tahrir ya Afrika ya mashariki, tawi la Zanzibar imesema CUF ndio chama kikuu cha upinzani kilitarajiwa kuikosowa serikali juu ya tatizo hilo, lakini kimekaa kimya. Taarifa ya jumuiya hiyo iliyotiwa saini na naibu katibu mkuu wake Sheikh Masoud Msellem imesema tatizo hilo lilipotokea mwaka 2008 chama cha CUF kilikuwa mkosowaji mkubwa, lakini hivi sasa kimekaa kimya huku bei ya chakula na bidhaa nyingine zikiongezeka kutokana na tatizo hilo. Aidha taarifa hiyo imesema tatizo la umeme katika kisiwa cha Unguja sio ukosefu wa raslimali, uchakavu wa mitambo au ukosefu wa utaalamu bali ni mfumo unaohitaji marekebisho. Huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja limesababisha usumbufu kwa wananchi ikiwemo uhaba wa maji safi na salama pamoja na kuathiri kwa shughuli zao za uchumi. 16

Advertisements