Archive for March, 2010

MBUNGE WA CHAMA TAWALA CCM AJIENGUA

Na Juma Abdala-Zenj fm

DAR ES SLAAM:

Mbunge wa CCM jimbo la Kishapu mkoani Sinyanga Fred Mpendazoe amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha Jamii cha CCJ kilichoanzishwa hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema uwamuzi wake huo umekuja baada ya kutorishwa na CCM na kushindwa kushughulikia masuala muhimu ya vitendo vya ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka.

Amesema mambo mengine aliyotaja mbunge huyo ni ukodishwaji kampuni moja kwa ajili ya kufua umeme wa dharura ya Richmond na kudai masuala kama hayo yamefunikwa na chama tawala.

Hata hivyo mwanasiasa huyo amesema yuko tayari kukabiliana na changamoto zozote zitakazo ibuka na kusema hajutii kulikosa bunge lijalo ambalo ni la mwisho kabla ya kuvunjwa…..CLIPS….(SAVED-FRED)

Aidha bw. Mpandazoe amesema yeye ni kama mtangulizi wa kundi jingine kubwa la wana CCM watakao kihama chama hicho.

……2…DAR ES SALAAM…

DAR ES SALAAM….2..

Akizungumzia kuondoka kwa viongozi hao naibu mkuu wa kitengo cha propaganda na uenezi wa CCM Tambwe Hiza amesema iwapo wanachama hao watakihama itakuwa ni jambo la kusherehekea kwa vile chama hicho itakuwa kimemaliza matatizo yake….CLIPS…(SAVED-HIZA)

Kuhama kwa mbunge huyo kumekuja baada ya chama cha CCJ kidaiwa kuundwa na baadhi ya viongozi wandamizi wa CCM wanaodhaniwa kukosa ungwaji mkono na chama chao katika nafasi za kugombea ubunge kutokana na misimamo yao ya kuituhumu serikali ya chama tawala.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 71 mbunge anapojitoa katika chama kilichomuweka bungeni moja kwa moja anapoteza ubunge na hawezi kulipwa marupurupu yake.

25

Advertisements

CCM HAITAKUFA KWA KUANZISHWA SERIKALI YA MSETO Z’BAR-WAZIRI

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Waziri wa nchi afisi ya rais katiba na utawala bora Ramadhan Abdala Shaaban amesema chama cha Mapinduzi CCM hakiwezi kufifia kwa kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa Zanzbiar na badala yake kitaendelea kuimarika.

Akichangia muswada wa sheria wa kuanzisha kura ya maoni katika baraza la wawakilishi amewataka wafuasi wa CCM wenye mawazo hayo waondokane nayo na kukubali kubadilika katika Nyanja za kisiasa.

Hata hivyo waziri Shaaban ametaka kutolewa elimu zaidi kwa wananchi juu ya umuhimu wa kura ya maoni itakayotoa ridhaa kwa wananchi kukubali au kukataa mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa…….CLIPS……(SAVED-RAMADHAN)

Nae mwakilishi wa Jimbo la Ziwani Rashid Suleiman Seif ameiomba serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la vyeti vya kuzaliwa lililosababisha baadhi ya wananchi kukosa vitambulisho vya ukaazi na hatimae kushindwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.

……2…ZANZIBAR……

ZANZIBAR…….2

Amesema vijana wengi hasa wale wanaochipukia wameshindwa kuandikisha katika daftari hilo kutokana na kukosa vyeti vya kuzaliwa, hivyo hatua hiyo pia inaweza kuwakosesha kupiga kura ya maoni…..CLIPS…..(SAVED-RASHID)

Muswada huo ni matokeo ya azimio la wajumbe wa baraza la wawakilishi waliotoa katika kikao cha mwezi Januari mwaka huu mabapo waliotoa mapendekezo ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa

19

MASHEHA WAONYWA NA MRAJISI MKUU WA SMZ

ZANZIBAR:

Afisi ya mrajisi mkuu wa serikali imewatahadharisha masheha wasiokuwa waminifu wanaweza kusababisha raia wa kigeni wakiwemo wasomalia kupatiwa vyeti vya kuzaliwa vya Zanzibar.

Mkuu wa afisi hiyo Abdala Waziri amesema afisi yake imekuwa akipokea barua kutoka kwa baadhi ya masheha kutaka kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa watu waliokuwa hawajazaliwa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliojadili umuhimu wa kuwa na kadi za uraia wa Tanzania huko Pwanimchangani bw. Waziri hakutoa takwimu halisi za kesi za ainai hiyo kwa mwaka lakini amesema ubabishaji huo unaofanywa na baadhi ya masheha unaweza kuhatarisha hali ya usalama nchini.

Hata hivyo amesema afisi hiyo haina uwezo wa kuwachukuliwa hatua za kinidhamu masheria hao kwa vile wako chini ya wizara nyingine, lakini kesi za aina hiyo zinawasilishwa katika wizara husika.

……2….ZANZIBAR…….

ZANZBIAR…..2..

Kuhusu suala la kukosa vyeti vya kuzaliwa kwa baadhi ya wananchi kisiwani Pemba ambao wamekosa vitambulisho vya ukaazi bw. Waziri amesema afisi yake imeandaa utaratibu maalumu wa kuwapatia watu hao vyeti hiyo.

Amefahamisha kuwa utaratibu huo tayari umeanza kutumiwa na baadhi ya wananchi waliokuwa hawana vyeti vya kuzaliwa wamepatiwa na hatimae kusajiliwa katika afisi za vitambulisho vya ukaazi.

MPANGO WA SMZ WA MABADILIKO YA SERIKALI ZA MITAA NI KUONGEZA GHARAMA ZA MATUMIZI-WANASIASA

ZANZIBAR:

Baadhi ya viongozi wa siasa na jumuiya za kiraia wamesema mpango wa serikali wa kutaka kuleta mageuzi ya serikali za mitaa unaweza kuliongezea taifa gharama za matumizi.

Wamesema wigo wa kuleta maendeleo kwa Zanzibar ni mzuri, lakini mpango huo wa kuimarisha madaraka mikoani unahitaji kufanyiwa utafiti wa kina ili serikali isijiingize katika matumizi yasiokuwa ya lazima.

Wakizungumza katika kongamano la kuharakisha mageuzi ya serikali za miataa, viongozi hao wamesema Zanzibar bado ni ndogo na serikali kuu inaweza kuwafikia wananchi wake wote…..CLIPS….(SAVED-MDAHALO)

Nae diwani wa wadi ya Mfanesini Msimu Said Abdala amesema madiwani wana kazi ngumu, lakini hawalipwi mishara, viinua mgongo na kutopatiwa vitendea kazi na ofisi.

Hivyo amehimiza uongozi wa sasa wa serikali za mitaa unahitaji kufanyiwa mageuzi ya sheria yatakayotoa umuhimu wa kuthaminiwa uwajibikaji wa madiwani kwa wananchi wanao waongoza…LIP…..(SAVED-DIWANI)

Mdahalo huo wa siku moja uliofanyika huko Eacrtanal mjini hapa umetayarishwa na Muungano wa jumuiya zisizo za kiserikali ANGOZA na kuwashirikisha wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na viongozi wa jumuiya za kiraia.                                18

KARUME AHIDI UMEME WA HAKIBA IFIKAPO JUNE 2010,

ZANZIBAR:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema hatua za awali za utekelezaji wa mradi mpya wa uzalishaji wa umeme wa dharura zimeanza kuchukuliwa kwa kushirikiana washirika wa maendeleo.

Amesema mradi huo unakusudia kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme wa dharura wa Megawati 45 katika eneo la Mtoni litakalokuwa na majenereta ya akiba 32 yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 25 sawa na asilimia 60 ya mahitaji.

Akitoa shukrani kwa wanachi kufuatia kukosekana kwa huduma ya umeme kwa miezi mitatu iliyopita rais Karume amesema nchi za Norway, Sweden na Uingereza zimechangia Dola za Kimarekani Milioni 11.50 na serikali imetoa dola milioni 1.50 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Amesema mikataba yote imeshatiwa saini na hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo zimeanza na unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu kwa mitambo hiyo kuzalisha umeme wa dharura.

…..2…..ZANZIBAR…..

ZANZIBAR……2

Kuhusu mradi wa uwekaji wa waya mpya umeme kutoka Tanzania bara hadi kisiwa cha Unguja utakaofadhiliwa na Marekani kupitia shirika la Changamoto la Millenia MCC rais Karume amesema mradi umefikia katika hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika na kuanza kazi  mwaka 2012.

Amesema mradi huo wenye uwezo wa Megawati 100 utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 84 ambapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itatoa shilingi bilioni nne.

Kuhusu mradi wa umeme wa uhakika kutoka Tanga hadi Pemba rais Karume amesema utekelezaji wake umefikia katika hatua nzuri na mwisho wa mwezi wa Aprili kisiwa hicho kitapata umeme wa uhakika.

Mradi huo umegharimu dola za Kimarekani milioni 75 ambapo serikali ya  Norway imechangia Dola milioni 60. Serikali ya Muungano Dola milioni tano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dola milioni 10.

Rais Karume amsema juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaiwezesha Zanzibar kuwa na miundo mbinu ya umeme wa uhakika kwa kipindi cha miaka ijayo, pamoja na mawasiliano ya kisasa.

Hatua hiyo itatoa nafasi kwa serikali na wananchi kushughulikia uwekezaji katika miradi mbali mbali ya kiuchumi na uimarishaji wa huduma za jamii inayohitajia nishati ya umeme.                                31

CUF YAMUOMBA KARUME KUSHUGHULIKIA VITAMBULISHO

ZANZIBAR: Chama Cha Wananchi CUF kimemuomba rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume kushughulikia tatizo la upatikanaji wa vitambuilisho vya ukaazi kwa baadhi ya wananchi. Chama hicho kimesema baadhi ya watu wamekosa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na kukoseshwa vitambulisho vya ukazi. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CUF Salim Bimani ametoa ombi hilo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho huko Masumbani Wilaya ya Mjini. Amesema masheha wamekuwa wakiwanyima wananchi barua ya kuombea vitambulisho hivyo katika afisi ya vitambulisho vya ukaazi na kumtaka rais Karume kuingilia kati suala hilo….CLIPS….(SAVED-BIMANI) Nae Naibu Katibu Mkuu wa CUF Juma Duni Haji amesema hakuna mtu anaeweza kuyazuwia mabadiliko ya kisiasa na kuitaka afisi ya vitambulisho vya ukaazi kuwapa wananchi vitambulisho hivyo bila ya kujali itikadi zao za kisiasa…….CLIPS…….(SAVED-DUNI) 15

SHIRIKA LA UMEME LATARAJIA KUFANYA MGAO

Na Juma Abdala Ali -ZEnji Fm

UNGUJA: Baada ya kurejea huduma ya umeme katika kisiwa cha Unguja Shirika la umeme Zanzibar limesema litalazimika kuanza mgao wa umeme endapo watumiaji wa huduma hiyo hawatapunguza matumizi yasiokuwa ya lazima. Akizungumza na Zenji Fm radio kaimu meneja mkuu wa shirika hili Hassan Ali Mbarouk amesema uwezo wa Cable inayoleta umeme kutoka Tanzania bara ni megawati 40 na iwapo matumizi yakizidi kwa kiwango kikubwa shirika litalazimika kuanza mgao huo. Hivyo amewataka watumiaji kupunguza matumizi yasiokuwa ya lazima katika kipindi cha kuanzia saa 1.00 hadi 4.00 ili kusaidia kuepukana na mgao wa umeme. Aidha amesema jenerata zinazotarajiwa kuongeza kiwango cha umeme zitawasili nchini hivi karibuni…….CLIPS……(SAVED-UMEME) Huduma ya umeme iliyoanza kurudi jana baada ya kipindi cha miezi mitatu mfululizo kukosekana bado haijawa katika hali ya kawaida kutokana na kukatika mara kwa mara katika baadhi ya maeneo. 15