ZANZIBAR:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume amesema hatua za awali za utekelezaji wa mradi mpya wa uzalishaji wa umeme wa dharura zimeanza kuchukuliwa kwa kushirikiana washirika wa maendeleo.

Amesema mradi huo unakusudia kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme wa dharura wa Megawati 45 katika eneo la Mtoni litakalokuwa na majenereta ya akiba 32 yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 25 sawa na asilimia 60 ya mahitaji.

Akitoa shukrani kwa wanachi kufuatia kukosekana kwa huduma ya umeme kwa miezi mitatu iliyopita rais Karume amesema nchi za Norway, Sweden na Uingereza zimechangia Dola za Kimarekani Milioni 11.50 na serikali imetoa dola milioni 1.50 kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Amesema mikataba yote imeshatiwa saini na hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo zimeanza na unatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu kwa mitambo hiyo kuzalisha umeme wa dharura.

…..2…..ZANZIBAR…..

ZANZIBAR……2

Kuhusu mradi wa uwekaji wa waya mpya umeme kutoka Tanzania bara hadi kisiwa cha Unguja utakaofadhiliwa na Marekani kupitia shirika la Changamoto la Millenia MCC rais Karume amesema mradi umefikia katika hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika na kuanza kazi  mwaka 2012.

Amesema mradi huo wenye uwezo wa Megawati 100 utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 84 ambapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itatoa shilingi bilioni nne.

Kuhusu mradi wa umeme wa uhakika kutoka Tanga hadi Pemba rais Karume amesema utekelezaji wake umefikia katika hatua nzuri na mwisho wa mwezi wa Aprili kisiwa hicho kitapata umeme wa uhakika.

Mradi huo umegharimu dola za Kimarekani milioni 75 ambapo serikali ya  Norway imechangia Dola milioni 60. Serikali ya Muungano Dola milioni tano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dola milioni 10.

Rais Karume amsema juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaiwezesha Zanzibar kuwa na miundo mbinu ya umeme wa uhakika kwa kipindi cha miaka ijayo, pamoja na mawasiliano ya kisasa.

Hatua hiyo itatoa nafasi kwa serikali na wananchi kushughulikia uwekezaji katika miradi mbali mbali ya kiuchumi na uimarishaji wa huduma za jamii inayohitajia nishati ya umeme.                                31

Advertisements