Archive for April, 2010

ABIRIA WAZILALAMIKIA MELI ZA ABIRI ZANZIBAR

ZANZIBAR:

Vyombo vya usafiri wa majini vya abiria vinavyofanya safari kati ya Dar es salaam na Zanzibar vimelalamikiwa na wananchi wa Zanzibar kutokana na tabia ya kujaza abiria kupita kiasi na kutishia usalama wa abiria.

Akizungumza na Zenj Fm radio juu ya malalamiko hayo mrajisi wa meli Zanzibar Abdalah Mohamed amesema meli zinazofanya safari kati ya Dar es salaam na Zanzibar zimekuwa zikikaguliwa mara kwa mara.

Amesema meli hizo zinapokuja  Zanzibar kabla ya kusajiliwa ni lazima ikaguliwe na kufuata taratibu zote za huduma za usafiri wa baharini ili zipewe kibal.

Akizungumzia suala la uzidishaji wa abiria ambalo linaonekana kutokea mara kwa mara amesema meli kikawaida inaweza kuzidisha abiria kutokana na sababu maalum ikiwemo wakati wa sherehe.

Hivi karibuni meli ya Flying Hourse iliripotiwa kuzidisha abiria ikiwa katika bandari ya Malindi ambapo abiria waliokuwa katika meli hiyo walipata hofu na hivyo kulazimika kurudi tena bandari wakati nahodha wa meli ya Sea Bus alipandishwa mahakamani kwa kosa kama hilo.

15

Advertisements

MKUU WA WILAYA YA WATE AGIZA KUFUKUZWA KAZI WAFANYAKAZI WAWILI WA HOSPITALI YA WETE BAADA YA KUTOA MANENO MACHAFU KWA MAMA MJAMZITO

PEMBA:

Mkuu wa wilaya ya Wete Omar Khamis Suleiman ameagiza kusimamishwa kazi wafanyakazi wawili wa hospitali ya Wete baada ya kumtolea lugha chafu mama mjawazito aliekwenda kujifungua katika hospitali hiyo.

Hatua ya kusimamishwa kazi kwa wafanyakazi hao imekuja baada ya mama mjamzito huyo ambae ni mke wa mkuu wa wilaya hiyo kutolewa lugha chafu na wafanyakazi hao wakati alipokwenda kujifunugua.

Akizungumza na mwandishi wetu kisiwani Pemba Bw. Suleiman amesema wafanyakazi wa hospitali hiyo wanaowapokea wagonjwa wanawatolea lugha chafu wagonjwa wakati wanapotaka kupatiwa matibabu na kuwafanya kuichukia hospitali hiyo.

Amesema lugha kama hizo sio nzuri na kusema yeye mwenyewe amezigundua na kuagiza hatua za kusimamishwa kazi zichukuliwe na uongozi wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Amefahamisha kuwa serikali yake itaendelea kuchukua hatua kama hizo kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya vingine  hasa maeneo ya vijijini kutokana na vitendo vya aina hiyo kukithiri.

Nae katibu wa hospitali ya Wete Salim Mohammed amesema amezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwa kuwaona baadhi ya wafanyakazi wanakiuka maadili ya kazi na kusema wataendelea kuwaelimisha ili kukomesha vitendo hivyo viovu.

Tukio kama hilo limesharipotiwa kutokea katika hospitali za Pemba ambapo wagonjwa wanadai kunyanyaswa na wafanyakazi wa hospitali.

22

WATU 20 WAHOFIWA KUFA MAJI MTWARA

MTWARA:

Zaidi ya watu 20 wanahofiwa kufa maji mkoani Mtwara baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama baharini.

Mashua hiyo inayokadiriwa kuwa na watu 28 imezama leo mchana karibu na pwani ya mji wa Mtwara.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo amesema hadi sasa mtu mmoja amekufa kati ya wanane waliokolewa na wengine 20 hawajulikani waliko  Habari zinasema wakati waokowaji wakiendelea na shughuli za uokozi mmiliki wa mashua hiyo amekimbia pamoja na nahodha wake.

MILLENIUM CHALLANGE YATIA SAINI KUISAIDIA ZANZIBAR NISHATI YA UMEME

Na Muzne Haji-Zanji Fm

ZANZIBAR:

Ofisi ya changamoto Milenium Tanzania leo imetiliana saini mkataba na kampuni ya Viscass  ya Japani ili kuanza utekelezaji wa mradi wa uwekaji wa waya wa umeme wa megawati 100 kutoka Tanzania bara hadi Zanzibar.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo ikulu mjini Zanzibar mtendaji mkuu wa Ofisi ya Changamoto Benard Said Mchomvu amesema mradi huo utasaidia maendeleo ya Zanzibar hasa katika sekta ya uwekezaji.

Amesema mradi huo utakaogharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 66.3 wakati serikali ya Zanzibar itatoa dola milioni 3.1 unatarajiwa kumalizika Disemba 2012 kwa ulazaji wa waya chini ya bahari ujenzi wa vituo utakaotengenezwa nchini Japan

Nae waziri wa maji ,ujenzi nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema mradi huo utaondoa tatizo la umeme katika kisiwa cha Unguja  na kuwasaidia wananchi katika juhudi za kupambana na umasikini.

Hafla hiyo ya utiaji saini pia imeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Aman Karume na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt pamoja na viongozi wa vyama na serikali.                                                15

SIKU MOJA KABLA YA MEI MOSI SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ZANZIBAR YAITAKA SMZ KUTATUA MATATIZO YA WAFANYAKAZI

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar Khamis Mwinyi Mohammed amesema bado wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi Zanzibar wanaendelea kukabiliwa na matatizo mbayo serikali inawajibika kuyashughulikia.

Akizungumza siku moja baada ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kufanyika hapo kesho amesema pamoja na mafanikio yaliopatikana kwa wafanyakazi katika kipindi hiki, lakini bado wanakabiliwa na matatizo ya mishahara midogo ya kima cha chini, pensheni ndogo kwa wafanyakazi wanaostaafu na marekebisho ya mishahara yasiozingatia hali ya maisha.

Aidha katibu mkuu huyo amewataka wafanyakazi kuwachagua viongozi watakaojali maslahi ya wafanyakazi katika uchaguzi mkuu ujao.

Amesema wafanyakazi wasifanye makosa kwa vichagua vyama au viongozi wasiojali maslahi yao.

Na huko Tanzania bara shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limesema kufanya au kutofanya mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima wa kudai maslahi yao utategemea mazungumzo yao yanaoendelea na serikali.

Shirikisho hilo linakusudia kuitisha mgomo wa wafanyakazi wa nchi nzima Mei tano mwaka huu endapo serikali haitayapatia ufumbuzi madai ya wafanyakazi ya kuongeza maslahi yao.

Siku ya wafanyakazi duniani hudhimisha kila ifikapo Mei Mosi ya kila mwaka na kutoa fursa kwa wafanyakazi kutathimini na kutafakari maslahi na matatizo wanayokabiliana nayo katika sehemu za kazi.

RAIS KARUMA ANATARAJIWA KUHUDHURIA UTIAJI WA SAINI WA UWEKAJI WA WAYA MPYA WA UMEME WA MEGAWATI 100 UNAOFADHILIWA NA SHIRIKA LA MILLENIUM CHALANGE

ZANZIBAR:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa utengenezaji wa waya mpya wa umeme wa chini ya bahari wa megawati 100 kutoka Tanzania bara hadi Zanzibar.

Mkataba wa utekelezaji wa mradi huo utatiwa saini ikulu mjini hapa kati ya kampuni ya VISCAS ya Japan iliyoshinda tenda ya utengenezaji na uwekaji wa waya huo na afisi ya Changamoto za Milenia Tanzania inayofadhili mradi huo.

Taarifa iliyotolewa na afisi ya Chamoto za Milenia kwa vyombo vya habari imesema balozi wa Marekani nchini Tanzania pia atahudhuria utiaji wa saini huo na viongozi wengine wa serikali ya mapinduzi Zanzibar na taasi ya Changamoto.

Kukamilika kwa mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 28 kutakiwezesha kisiwa cha Unguja kupata umeme wa uhakika ambao utachangia shughuli za uwekezaji.

Hivi karibuni waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid amesema kisiwa cha Unguja bado kinakabiliwa na tatizo la umeme licha ya matengenezo makubwa yalifanywa kwenye waya wa sasa unaoleta umeme kutoka Tanzania bara.

Amesema waya huo wa megawati 45 licha ya kumalizika muda wake, umezidiwa na matumizi na kuwataka wananchi kujiepusha na matumizi yasiokuwa ya lazima.

BADEA NA SAUD ARABIA FUND WAAHIDI KUISAIDIA ZANZIBAR UJENZI WA MIUNDO MBINU IKIWEMO UWANJA WA NDEGE WA PEMBA

ZANZIBAR:

Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika BADEA na Mfuko wa Saudi Arabia zimeahidi kuendelea kuisaidia Zanzibar katika ujenzi wa miundombinu ya barabara na mategenezo ya uwanja wa ndege wa Pemba.

Uongozi wa taasisi hizo za kifedha umetoa ahadi hizo ulipokuwa na  mazungumzo na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume, Ikulu mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo uongozi huo ulieleza kuwa tayari barabara zote tatu za Pemba zikiwemo barabara ya Wete-Gando, Wete-Konde na Chake -Wete ambazo wanazigharami zimo katika mpango wa ujenzi.

Aidha, taasisi hizo pia zimeelezea  nia yao ya kugharamia ujenzi wa barabara za Mwera-Pogwe-Jumbi, Cheju-Unguja Ukuu na Miwani-Kizimbani.

Nae rais Karume amesem serikali katika kuimarisha sekta ya mawasiliano ikiwemo miundombinu ya barabara pia, imeweka mikakati ya kuimarisha sekta ya kilimo hasa cha umwagiliaji maji.

Benki ya BADEA inaendelea kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA huko Tunguu wilaya ya Kati ambapo kukamilka kwa ujenzi  huo kutasaidia kuimarisha sekta ya elimu nchini.

Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza a Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akisalimiana  na Kiongozi wa Mfuko wa Saudi Arabia,(SOUD FUND),Ibrahim M.Alsugair pamoja na Viongozi Ujumbe Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika,(BADEA)walipofika Ikulu Mjini Zanzibar