Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa yanaweza kutoa fursa ya kuirejesha Zanziar katika hadhi yake ya zamani kuwa kituo kikuu cha biashara kwa nchi za Afrika mashariki na kati.

Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema fursa za kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikuu cha biashara ni kubwa na muhimu lakini kunahitaji mipango endelevu na yenye utulivu wa nchi.

Akiakhirisha kikao cha baraza la wawakilishi amesema Zanzibar ilitumia muda mwingi wa malumbano ya kisiasa yasiokuwa na msingi na kusahau jukumu la kujenga nchi.

Amesema serikali inaamini Zanzibar mpya ijayo inaweza kuwa na fursa ya kuwa kituo kikuu cha mawasiliano na usafiri wa angani na baharini hali ambayo itatoa fursa kwa wakezaji wakubwa kuja kuekeza nchini….CLIPS…..(SAVED-BIASHARA)

Aidha waziri kiongozi amesema Zanzibar inaweza kuwa kituo maalum kwa jaili ya uwekezaji wa mafuta ya ndege kubwa za mizigo na abiria na hata kuwa kituo maalumu cha kuegeshea ndege za kimataifa.              15

Advertisements