Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewakemea baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa wanaopita majimboni kueneza siasa chafu dhidi ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha amesema uwamuzi wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa bado haujatolewa na kusema suala hilo linahitaji maamuzi ya wananchi wenyewe kupitia kura ya maoni.

Akiahirisha kikao cha baraza la wawakilishi, amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanatumia sera za vyama vyao kupotosha ukweli wa kundwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema chama cha mapinduzi hakijafanya uamuzi wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa vile kinasuibiri maoni ya wananchi watakayoyatoa katika kura ya maoni na utekelezaji wake utafanyika baada ya uchaguzi mkuu wa 2010…..CLIP….(SAVED-NAHODHA)

…2…ZANZIBAR……

ZANZIBAR……2

Kauli hiyo ya waziri kiongozi imekuja kufuatia baadhi ya wanachama na viongozi wa vyama vya siasa kudaiwa kupita majimboni kuwataka wananchi wasikubali kupiga kura ya ndio katika kura ya maoni ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini.

Aidha waziri kiongozi Nahodha amesema ukurasa mpya wa maridhiano ya kisiasa Zanzibar utasaidia katika kuleta maendeleo na kusema wale wenye nia ya kuvuruga maridhiano hayo hawatapata nafasi.

Kikao cha baraza la wawakilishi kimeahirishwa hadi tarehe tisa June ambacho kitakuwa kikao cha mwisho kitakachojadili bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 kabla ya kuvunjwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu.

23

Advertisements