Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amekamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi 94 waliobomolewa nyumba zao zaidi ya miaka 30 iliyopita ili kupisha ujenzi wa nyumba za maendeleo za Michenzani.

Kumalizwa kwa idadi ya watu hao wanaodai fidia kumekuja baada ya kumaliza ujenzi wa nyumba ya maendeleio ya Michenzani nambari 10 ambapo ugawaji wake ulifanywa leo na rais Karume mbeli ya nyumba hiyo.

Rais Karume amesema licha ya nyumba hiyo kuwa na nafasi 182, lakini amepokea maombi 450 ya wananchi wanaotaka kupatiwa nyumba na kusema umuhimu utatolewa kwa vikosi vilivyoshiriki ujenzi wa nyumba hiyo na zitakazosaliwa watapewa wale wenye mahitaji ya msingi kwa njia ya mkopo………CLIPS…….(SAVED-AMANI)

Aidha rais Karume amewapongeza wananchi waliobomolewa nyumba zao kwa kuonyesha ustahamilivu mkubwa huku wakisubiri serikali kuwalipa haki zao.

….2…KARUME…..

KARUME…….2….

Amesema seriakali  inayo uwezo mkubwa wa kuwaletea maendeleo wananchi wake na kuwapatia makaazi bora iwapo kutakuwa na umoja na mshikamano miongoni mwa Zanzibari.

Amesema wale wanaotaka kupotosha malengo ya chama kilichoikomboa Zanzibar cha ASP ya kuleta maslahi bora kwa wanayonge hawatafanikiwa kutokana na mshikamano uliopo.

Rais Karume ameitumia nafasi hiyo kwa kuwashukuru wananchi waliompa imani ya kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha mihula miwili itakayofikia kikomo chake baada ya kufanyika uchaguzi Octoba mwaka huu.

Kumalizika kwa ujenzi wa nyumba na kulipwa fidia kwa wananchi waliobomolewa nyumba zao kunatokana na ahadi iliyotolewa na rais Karume wakati wa kampeni zake za kuwania uraisi wa Zanzibar.

Ujenzi wa nyumba hiyo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni 165 kati ya hizo shilingi bilioni moja ni mkopo kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii, Zanzibar ZSSF                                28

Advertisements