Na Juma Abdala-Zenji Fm

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema maridhiano ya kisiasa na dhana ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar utapunguza siasa za chuki, uhasama, vurugu na kushambuliana.

Amewataka wananchi kuunga mkono uwamuzi huo na kujitokeza katika upigaji wa kura ya maoni na kuunga mkono serikali ya umoja wa mataifa kwa vile ni jambo lenye maslahi kwa taifa.

Akipokea matembezi ya vijana wa CCM ya kumuenzi marehemu Abeid Amani Karume huko Maisara rais Kikwete ametaka wanaopotosha dhamira hiyo wasipewe nafasi na kuwataka viongozi wa CCM kuunga mkono uwamuzi wa chama chao wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

Amesema uwamuzi huo haukuwa rashi kwa CCM wala chama cha wananchi CUF na kusema kama ndiowenye maslahi kwa Zanzibar haunabudi utekelezwe kwa wakati huu ili kuleta maslahi kwa wananchi.

Rais Kikwete amsema mazingira ya ushindiani wa kisaisa na matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yamesababisha kufikia uwamuzi wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo italeta maslahi kwa taifa…..CLIPS….(SAVED-KIKWETE)

…..ZANZIBAR…2….

ZANZIBAR…..2…

Akizungumzia suala la uchaguzi mkuu ujao rais Kikwete amesema uchaguzi huo utakuwa bora zaidi ikilinganishwa na chaguzi nyingine kutokana na kuwepo sheria mpya ya gharama za uchaguzi itakayowezesha wagombea kuchaguliwa kwa sifa zao badla ya kutumia fedha au kununua wapiga kura.

Amesema sheira imeweka utaratibu mzuri wa kuongoza na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha, hivyo amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kuhamisishana kutoufanya uongozi kuwa ni kitu cha kununuliwa.

Aidha rais Kikwete amesema sheria hiyo itawahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao.

Matembezi hayo ya sita kumuenzi marehemu Karume yaliowashirikisha vijana 150 kutoka mikoa 26 ya Tanzania yalianzia kijiji cha Makunduchi Mkoa wa kusini Unguja, kupitia vijiji vya Mkoa wa kaskazini unguja na kuishia leo katika viwanja vya Maishara mkoa wa mjini maghairibi.

30

Advertisements