DAR ES SALAAM:

Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano Tanzania Samuel Sitta amesema kuna umuhimu wa kuweka wazi mpango wa kutangaza mali kwa viongozi ili kufanikisha dhana ya uwazi na kupambana na vitendo vya ufisadi mingoni mwao.

Akizindua mpango wa pili wa kulinda na kuhifadhi maadili ya umma unaoendeshwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam amesema mpango wa kutangaza mali za viongozi wa umma kwa sasa unafanyika kwa siri na kujaza fomu maalum.

Spika Sitta amesema hali hiyo inanyima umma fursa ya kufahamu mali walikozipata na hivyo kuondoa dhana nzima ya viongozi hao wa umma  kutangaza mali zao…..CLIPS…..(SAVED-SITTA)

Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimeamuwa kuendesha mpango huo hasa nyakati hizi za maadili kwa wananchi wakiwemo viongozi yamelezewa kuporomoka kwa kiasi kikubwa.

13

Advertisements