DAR ES SALAAM:

Serikali ya Tanzania imekanusha na kutoa msimamo wake dhidi ya shutuma zilizotolewa na upande wa upinzani visiwani Comoro katika kushughulikia hali tete ya kisiasa visiwani humo imekuwa ikipendelea serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Mohammed Sambi.

Waziri wa mambo ya nje na ushrikiano wa kimataifa Benard Membe amesema kutokana na hali tete nchini humo, Tanzania itaendelea kusimamia maamuzi yaliofikiwa na wengi.

Amesema Tanzania itaheshimu maamuzi ya bunge la nchi hiyo yanayotaka uchaguzi wa rais na magavana kisiwani Comoro ufanyike mwakani Novemba 11.

Visiwa vya Comoro ambavyo kila mwaka vimekuwa na chaguzi viko katika vugu vugu la kisiasa baada ya bunge la nchi hiyo kupitisha uwamuzi wa kuwa na uchaguzi mkuu mmoja unaotarajiwa kufanyika mwakani baada ya mwaka huu hatua ambayo inapingwa na upinzani.

13

Advertisements