PEMBA:

Msitu wa aina ya mkoko uko hatarini kutoweka kisiwani Pemba kutokana na matumizi mabaya ya ukataji wa miti hiyo unaofanywa na baadhi ya wananchi bila ya kufuata taaluma inayotolewa na idara ya misitu

Meneja Sekta ya Uhifadhi Mikoko Pemba Salim Khamis Haji amesema mikoko ina mchango mkubwa katika kuhifadhi mazingira ya ukanda wa pwani, hivyo iwapo itaendelea kukatwa kuna uwezekano mkubwa wa maji ya bahari kuendelea kupanda juu.

Amesema maeneo ya Mkoa wa Kaskazini Pemba yanaongoza katika ukataji wa mikoko kwa shughuli za kijamii na uchumi ikiwemo uzalishaji wa chumvi na ujenzi wa hoteli za kitalii.

Meneja huyo amesema mikoko ina umuhimu mkubwa kwa maisha ya hivyo ametoa wito kwa wananchi kupanda kwa wingi ili kuendeleza ukuaji wa msitu huo kwa lengo la kutunza mazingira.

Advertisements