Na Juma Abdala-zenji fm

ZANZIBAR:

Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC inakusudia kufanya utafiti ili kujua sababu za kuwepo idadi ndogo ya watu waliojitokeza kujiandikisha katika daftri la kudumu la kupigia kura katika uchaguzi wa mwaka huu.

Mkurugenzi wa tume hiyo Salum Kassim amesema mwaka huu kumekuwa na idadi ndogo ya watu walijitokeza kuandikisha katika daftari hilo Zanzibar ikinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2005.

Akizungumzia kuhusu ushiriki mdogo wa wanawake kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu mwaka huu amesema kuna haja ya wanawake kuhamasishwa kushiriki katika kugombea nafasi hizo.

Amesema uchaguzi wa mwaka 2005 idadi ya wanawake waliopiga kura ilikuwa ni kubwa, lakini waliojitokeza kugombea nafasi za uongozi ilikuwa ndogo chini ya asilimia 30 ikilinganishwa na idadi ya wanaume

Advertisements