ZANZIBAR:

Kikundi kinachojiita Pressure Group G-12 kimemshauri rais Kikwete na rais Amani Karume kuunda timu maalum itakayoshughulikia matatizo ya muungano yanayoleta usumbufu kwa Zanzibar.

Mshauri wa kikundi hicho Amour Bamba ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kuhoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amesema timu hiyo itakayoteuliwa isiwe na watendaji wa serikali ambayo inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana ufumbuzi wa matatizo ya muungano yanayodaiwa kuwepo kwa muda mrefu.

Amezitaja baadhi ya kero hizo ni kutokuwepo usawa baina ya uteuzi wa utumushi wa serikali ya muungano pamoja na ugawanaji wa raslimali na misaada kutoka kwa wahisani. ……

Aidha bw. Bamba wananchi wa Zanzibar na Tanganyika wanapenda muungano,lakini amedai bado haujaelezwa wazi haki kwa kila pande hizo za muuungano

Hata hivyo kikundi hicho cha G-12 kimesema kimepeleka madai yao katika umoja wa mataifa kutaka kujua uhalali wa Muunguno.……

Advertisements