Na Juma Abdala-Zenji Fm

DAR ES SALAAM:

Watanzania leo wameadhimisha sherehe za miaka 46 tangu kuundwa Muugano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama Jakaya Mrisho Kikwete katika maadhimisho hayo amepokea na kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi hivyo na kupigwa mizinga 21.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na maelfu ya watanzania na viongozi wengine serikali na vyama vya siasa akiwemo rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na mabalozi wa nchi za nje waliopo Tanzania.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume na rais wa Tanganyika Mwalim Julius Kambarage Nyerere.

Miongoni mwa mambo muhimu yaliosababisha viongozi hao kuunganisha nch zao ni kutaka kuleta umoja wa bara zima la Afrika

Advertisements