DAR ES SALAAM:

Rais wa Marakani Barac Obama ametuma salamu za pongezi za miaka 46 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema matarajio yake ni kuona uhusiano wa nchi yake na Tanzania utazidi kuimarika.

Taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ikulu mjini Dar es Salaam imekariri taarifa ya balozi wa Marekani ikisema matarajio ya rais Obama ni kuona uhusiano wa nchi mbili hizo unazidi kuimarika.

Taarifa hiyo imesema rais Obama ana matumaini ya muungano  huo utaendelea kuleta mafanikio ya kudumu miongoni mwa watanzania.

Salamu nyingine za pongezi zimetoka na kiongozi wa madhehebu ya Ismailia duniani Aga Khan na kusema ataendeleza uhusiano na Tanzania katika kuchangia maendeleo ya nchi.

Advertisements