ZANZIBAR:

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar ZATUC linakusudia kuwashawishi wanachama wao kutochangia mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF kutokana na mfuko huo  kutotimiza  ahadi katika utoaji wa mafao ya uzazi na ugonjwa kwa wananchama wake.

Akizungumza na zenji fm radio katibu mkuu wa ZATUC Khamis Mwinyi Mohammed amesema mfuko huo kwa muda mrefu sasa umeshindwa kutoa mafao hayo huku ukiendelea kuwachanganisha wanachama wake.

Amesema kwa vile shirikisho lao lina mjumbe katika bodi ya ZSSF wanafikiria  kumtoa mjumbe huyo ili kuepuka kushirikishwa katika mpango huo wa ZSSF unaokwenda kinyume na sheria za kuanzishwa kwa mfuko huo kwa kukosa kulipa mafao hayo……CLIPS….(SAVED-ZSSF)

Hivi karibuni mkurugenzi wa Mfuko wa ZSSF Abdulwakil Haji amesema tatizo la kutolewa kwa mafao hayo linatokana na hali ya michango kwa wanachama wake kuwa midogo.

Hata hivyo Mfuko wa ZSSF ulioanzishwa mwishoni mwa mika ya 90 unaendelea kutoa mafao ya uzeeni kwa wananchama wake wanaostaafu kazi na kuwekeza miradi kadhaa ya kiuchumi pamoja na kutoa mikopo kwa taasisi mbali mbali nchini.                            17

Advertisements