DAR ES SALAAM:

Matokeo ya utafiti yaliofanywa na mpango wa elimu ya demokrasia wa chuo kikuu cha Dar es Salaam REDET juu ya maoni ya wananchi katika uchaguzi mkuu ujao yameonesha iwapo uchaguzi huo ungefanyika sasa chama cha Mapinduzi CCM kingeibuka na ushindi katika nafasi za urais, ubunge na madiwani.

Taarifa ya utatifi huo uliofanyika mwezi uliopita ilitolewa leo mjini Dar es Salaam kwa wandishi wa habari na mtafiti mkuu wa REDET Dr. Benerdeta.

Amesema asilimia 60 ya wabunge wa sasa wa majimbo wangalipoteza viti vyao kwa kutowajibika ipasavyo katika majimbo yao….CLIPS……(SAVED-BENADETA)

Aidha Dr. Benerdeta amesema vyama vya CUF na CHADEMA vimonekana ndio vyama pekee vyenye kuleta upinzani nchini.

Utafiti huo ulizihusisha wilaya 52 nchini, huku asilimia 60 ya wananchi waliohojiwa ni wakaazi wa vijijini na asilimia 40 ni wa mjini.

Lengo la utafiti huo nikuvisaidia vyama vya siasa kuangalia ilani zake ili kukidhi matakwa ya wananchi ambao ndio wapiga kura.            13

Advertisements