MKOA WA KUSINI UNGUJA:

Wizara ya kilimo, mifugo na mazingira imefanikiwa kupata mbegu mpya ya mpunga inayoweza kustawi katika maeneo ya uwandani na maweni.

Afisa wa kilimo katika mkoa wa kusini Unguja Ameir Haji Ameir amesema mbegu hiyo imepatikana baada ya utafiti uliofanywa katika kituo cha kilimo cha Makunduchi wilaya ya kusini.

Amesema kupatikana kwa mbegu hiyo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuimarisha sekta ya kilimo nchini hasa mpunga ili kuwa na chakula cha kutosha.

Ameir amethibitisha utafiti wa mbegu hiyo katika kipindi cha miezi mitatu umeonyesha mafanikio katika nchi za Afrika ikiwemo Uganda

Advertisements