Archive for May, 2010

SMZ KUSHAURIWA KUACHANA NA KODI ZA SIGARA

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kutafuta njia mbadala za kuingiza mapato ili kuondokana na mapato yatokanayo na kodi za makampuni ya siraga kutokana kuhatarishs afya za watumiaji.

Akizungumza na Zenji fm radio juu ya siku ya kukataza uvutaji wa sigara duniani afisa wa elimu wa kitengo cha dawa za kulevya Zanzibar Dr. Kassi Ali Simai amesema hasara inayotokana na sumu ya sigara kwa afya ya mwadamu ni kubwa ikilinganishwa na mapato hayo.

Amefahamisha licha ya serikali kukusanya mapato mengi kutoka makampuni ya sigara, lakini moshi wake una zaidi ya chemical 400 zinazohatarisha afya za watumiaji hivyo ni vyema kufikiria njia nyingine mbadala ya ukusanyaji wa mapato.

Dr. Simai amesema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na moshi wa sigara kwa kuugua homa ya ini na saratani

Katika kuadhimisha siku ya uvutaji wa sigara duniani shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, limevilaumu viwanda vya sigara  kwa kuwahamasisha wanawake katika nchi masikini kuvuta sigara.

Mtaalamu wa shirika hilo la WHO, Douglas Bettcher amesema, utafiti umeonesha idadi ya wanawake na vijana wanaovuta sigara katika  nchi masikini imekuwa ikiongezeka.

Advertisements

KARUME AMETOWA WITO WA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUUNDO WA SHIRIKA LA IMF

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Amani Abeid Karume akiwa katika ufunguzi wa mkutano wa WEF uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sheraton mjini Doha, Qatar, kushoto ni Waziri wa Maendeleo wa Taifa wa Singapore MAHBOW-TAN kulia kwa Rais ni Mwana wa Mfalme na Mwenyekiti wa Viongozi wa Vijana Duniani Mhe. HAAKON

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume ametowa wito wa kuwepo mabadiliko katika taasisi za kifedha za Kimataifa ili kuweza kutoa nafasi sawa katika mataifa yote makubwa na madogo ulimwenguni.

Rais Karume ametoa wito huo katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Kiuchumi Duniani (WEF) unaofanyika mjini Doha, Qatar.

Katika mkutano huo Rais Karume alisisitiza kuwa maendeleo ya uhakika hayawezi kupatikana bila ya kuwepo mageuzi ya kifedha ya kimataifa hasa kwa kzingatia kuwa taasisi hizo ziliudwa wakati ambao kulikuwa na nchi chache zenya uwezo wa kiuchumi na kiutawala duniani.

Alieleza kuwa wakati huo taasisi hizo ziliundwa kwa lengo la kukidhi mahitaji ya nchi hizo chache.

“Taasisi hizo ziliudwa ili kukidhi mahitaji hayo lakinisasa wadau ambao ni sisi sote tuko wengi na ni lazima kupatikana usawa wa fursa ili kuweza kushiriki kikamilifu”,alisema DK. Karume.

Aidha, Rais Karume alizungumia umuhimu wa elimu katika kuleta maendeleo ya binaadamu na kusisitiza haja ya kuiimarisha sekta hiyo.“Elimu ndio ufunguo wa maisha katika maendeleo ya binaadamu” alieleza Rais Karume.

Rais Karume alisisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano wa kimataifa katika maendeleo ya elimu.

Katika mkutano huo, Rais Karume  alkuwa ni miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika ufunguzi wa mkutano huo.

Miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo ambao ulifunguliwa na Amir wa Qatar Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani walikuwa ni mrithi wa Mfalme wa Norway  Prince Haakon, Mke wa Mfalme wa Jordan  Queen Rania, Waziri wa Maendeleo wa Singapore na wengineo.

Wazungumzaji wote wakuu katika mkutano huo walisisitiza haj ya kuimarisha sekta ya elimu kwani ndio mkombozi katika kuimarisha sekta zote za maendeleo na ukuzaji wa uchumi.

Amir wa Qatar Sheikh Hamad akifungua mkutano huo mkubwa wa kiuchumi duniani alisisitiza ushirikiano wa kimataifa na kubuni mikakati itakayosaidia katika kupambana kwa pamoja na matatizo ya kiuchumi duniani.

Aidha, nae mke wa Mfalme waa Jordan Queen Rania alizungumzia umuhimu wa maendeleo ya vijana hasa katika maendeleo ya elimu.

Queen Rania alieleza kuwa kukosekana kwa elmu kunasababisha ukandamizaji wa vijana na watoto sanjari na kukosa fursa za kujiimarisha kimaendeleo.

Ufunguzi wa mkutano huo uliendeshwa na Profesa Claus Schwab ambaye ndie Mwenyekiti Mtendaji wa WEF.

Mkutano huo ulitanguliwa na mikutao midogo midogo ya majadiliano juu ya mada mbali mbali zikiwemo elimu, afya, maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa, uimarishaji wa uchumi na fedha, mazingira, usalama na nyenginezo ambayo iliwashirikisha viongozi mbali mbali kutoka sekta tofauti za serikali na zile za kibinafsi wakiwemo mawaziri,wataalamu na wakuu wa taasisi tofauti ambapo Tanzania pia imewakilishwa na baadhi ya Mawaziri waliomo katika nyanja hizo

Wanaume wapendanao waachiwa Malawi

kutoka bbc

Wapenzi wa jinsia mojaWapenzi wa jinsia moja

Wanaume wawili wanaofanya mapenzi ya jinsia moja nchini Malawi waliofungwa baada ya kufanya sherehe ya uchumba wamesamehewa na Rais Bingu Wa Mutharika.

Bw Mutharika, akizungumza wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alipotembelea nchi yake, amesema ameamuru waachiliwe huru haraka iwezekanavyo.

Steven Monjeza na Tiwonge Chimbalanga walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela mapema mwezi huu kwa kufanya vitendo kinyume cha maumbile na vitendo vya aibu.

Kesi hiyo iliibua malalamiko kutoka nchi za kimataifa napia mjadala juu ya mapenzi ya jinsia moja ndani ya Malawi.

Bw Ban ameusifu uamuzi wa Rais kuwa ni wa “kijasiri.”

Amesema, “Sheria hii iliyopitwa na wakati irekebishwe popote ilipo.”

‘Utamaduni wa chuki’

Waandishi wanasema Malawi ni jamii yenye msimamo mkali sana ambapo viongozi wa dini huhusisha mapenzi ya jinsia moja na ushetani.

Bw Mutharika amewaachia huru kwa misingi ya haki za binadamu.

Baada ya kukutana na Bw Ban alisema, “Wanaume hawa wawili wametenda uhalifu dhidi ya mila zetu, dini zetu na sheria zetu.”

“Hata hivyo, kama mkuu wa nchi nawasamehe na hivyo waachiwe haraka iwezekanavyo bila masharti yeyote.”

Steven Monjeza, 26, na Tiwonge Chimbalanga, 20, walikuwa gerezani tangu walipokamatwa Desemba 2009 baada ya kufanya sherehe ya uchumba, kabla ya mipango ya kufunga ndoa mwaka 2010.

Gift Trapence, kutoka kituo cha kutetea maendeleo ya watu, amefurahiswa na uamuzi huo.

Amesema, “Tumefurahi sana na tunamsifu Rais kwa ukomavu wake, lakini bado tuna safari ndefu kumaliza mila hizi za chuki.”

Sheria za kikoloni

Mashirika ya kutoa misaada na haki za binadamu yamekuwa yakishinikiza serikali yake kuheshimu haki ya wachache.

Wanaume hawa wawili wametenda uhalifu dhidi ya mila zetu, dini zetu na sheria zetu.

Bingu Wa Mutharika, Rais wa Malawi

Serikali ya Uingereza, mfadhili mkuu wa Malawi, ilisema ilishtushwa na hukumu hiyo, na Marekani iliuelezea kama hatua moja nyuma katika harakati za kupigania haki za binadamu.

Siku ya Jumamosi, mwanamuziki wa miondoko ya Pop Sir Elton John aliandika barua ya wazi kwa Bw Mutharika kupitia gazeti la Uingereza la The Guardian akiomba waachiwe huru.

Wanaume hao wawili wamehukumiwa kwa sheria ya zamani ya kikoloni wakati Malawi ilipokuwa ikitawaliwa na Uingereza.

Makoloni mengi yaliyokuwa ya Uingereza yana sheria sawa na hiyo inayopinga mapenzi ya jinsia moja: India ilibadilisha sheria hiyo ya kuwapinga mwaka jana.

VITENDO VYA UHARAMIA VINAWEZA KUATHIRI UCHUMI WA Z’BAR-DR. MWINYIHAJI

Eneo la bandari ya Zanzibar

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwepo kwa vitendo vya uharamia kati ya visiwa vya Unguja na Pemba vinavyoripotiwa katika vyombo vya habari kunaweza kuathiri uchumi wa Zanzibar. Akizungumza na zenji fm radio juu ya athari za vitendo hivyo kwa uchumi wa Zanzibar waziri anaeshughulikia masuala ya fedha na uchumi Dr. Mwinyihaji Makame amesema licha ya kutopata uthibitisho wa vitendo hivyo, lakini Zanzibar ni sawa na nchi nyingine ziliomo katika ukanda wa bahari ya Hindi inaweza kuathirika kiuchumi kutokana na uharamia huo. Amesema iwapo meli za mizigo zinazotaka kuingia katika eneo la Afrika ya mashariki zinatishiwa na maharamia wa kisomali bila shaka hali ya uchumi wa Zanzibar itakuwa mbaya. Hata hivyo Dr. Makame amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kufanya doria za kuwasaka maharamia hao walioripotiwa kuwepo katika kisiwa cha Pemba. …CLIPS…(SAVED-MWINYIHAJI) Kazi ya kuwasaka maharamia hao wa kisomali bado zinaendelea kwa ushirikiano wa jeshi la polisi, vikosi vya SMZ pamoja na jeshi la wananchi Tanzania JWTZ. …….2…..ZANZIBAR………… ZANZIBAR….2……. Akizungumza na Zenji Fm Radio juu ya msako huo kamanda wa kikosi cha kuzuia magendo KMKM kisiwani Pemba amesema kuwa kazi inaendelea vizuri na hadi sasa wananchi wanatoa ushirikiano mzuri……CLIPS….(SAVED-KMKM) Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba. Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba

VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA TANZANIA WAWASAKA MAHARAMIA WA KISOMALI WALIOKIMBILIA PEMBA

PEMBA:

        Vikosi vya ulinzi na usalama vimeripotiwa kuweko katika msako mkali wa kuwatafuta maharamia wa kisomali wanaodaiwa kukimbilia kisiwani Pemba baada ya kushindwa kuiteka meli katika bahari kuu ya Tanzania.

        Kamanda wa polisi wa mkoa kusini Pemba Hassan Nassir amesema msako huo unavishirikisha vikosi vya SMZ na wanajeshi wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ.

Amesema taarifa za msako huo zitatolewa hapa baadae

        Msako huo umekuja siku moja baada ya kuripotiwa watu wanaodaiwa maharamia waliotaka kuiteka nyara meli moja katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania kukimbilia kisiwani Pemba.

        Maharamia hao wamekimbilia Pemba baada ya kushambuliwa na majeshi ya jumuiya ya umoja wa ulaya wanaofanya doria katika pwani ya Afrika ya mashariki wakitaka kuiteka meli kati kati ya bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU TUNGUU ZAIDI 300 WAMEFUKUZWA KWA KUSHINDWA KULIPA ADA

Na Juma Abdala-Zenji Fm

MKOA WA KUSINI UNGUJA: Wanafunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar, Tunguu mwaka wa pili, wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kuwafukuza baada ya kukosa kusajiliwa kwa kile kilichoelezwa kushindwa kukamilisha malipo ya ada. Akizungumza na Zenji Fm radio mmoja wa wanafunzi hao amedai chuo hicho kimeongeza ada ya masomo kinyume na mkataba wao wa zamani hivyo wameshindwa kulipa ada hiyo na kulazimika kufukuzwa. Amedai kutokana na kufukuzwa chuo kinyume na sheria wanatarajia kufungua kesi mahakamani wiki ijayo kutokana na kufukuzwa kwa zaidi ya wanafunzi 300…….CLIPS….(SAVED-TUNGUU) Hata hivyo uongozi wa chuo hicho haukuweza kupatikana kuelezea juu ya madai hayo ya wanafunzi kufukuzwa chuoni hapo

ANGOZA KUFANYA TAMASHA LA JUMUIYA ZA KIRAIA ZANZIBAR

Juma Abdala -Zenji Fm

ZANZIBAR: Jumuiya ya taasisi za kiraia ANGOZA imeandaa tamasha la siku mbili la maonyesho la asasi za kiraia za Zanzibar litakaloanza leo katika viwanja vya hoteli ya Bwawani. Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya hiyo John Ulanga amesema lengo la tamasha hilo litakalofuatiwa na mijadala ni kuzijengea uwezo taasisi za kiraia. Amesema pamoja na kuandaliwa kwa matamasha jumuiya hiyo pia imekuwa ikitoa ruzuku kwa wananchama wake ili kuona zinatoa huduma nzuri kwa wananchi. Akizungumzia masuala ya uchaguzi na taasisi za kiraia Ulango amesema taasisi hizo pia zitahamasishwa juu ya majukumu yao katika shughuli za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu. Jumuia ya taasisisi za kiraia Tanzania hii ni mara yake ya kwanza kuendesha tamasha kwa wananchama wake hapa Zanzibar kati ya matamasha saba iliyoyafanya katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Hata hivyo Jumuiya hiyo imekuwa ikiwashirikisha wanachama wake katika maonyesho ya kila mwaka yanayofanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi yakiwa na lengo la kusogeza huduma zao zaidi kwa wananchi. 18