DAR E SALAAM:

        Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameungana na viongozi wengine dunia kutuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa Nigeria kufuatia kifo cha rais Omar Yar’duwa aliefariki dunia  akiwa na umri wa miaka 58.

        Katika salamu hizo rais Kikwete amelezea kusitikishwa kwake na kifo hicho na kusema marehemu Yarduwa atakumbukwa kama kiongozi alieimarisha demokrasia nchini Nigeria.

Nae rais wa Liberia Allen Johnson Sarif amemtaja Yar’duwa kama kiongozi mtulivu, mwenye nidhamu aliejitahidi kuinua hali ya Afrika ya magharibi.

        Rais wa Marekani Barack Obama amesema Yar’dua atakumbukwa kama mkweli na mwenye hadhi pamoja na uwezo kwa wananchi wa Nigeria.

        Serikali ya Nigeria imetangaza siku saba za maendeleo kufuatia msiba huo.

        Yar’duwa amefarikdi dunia akiwa na umri wa miaka 58 alingia madarakani mwaka 2007.                       

Advertisements