DAR ES SALAAM:

        Mkutano wa dunia wa uchumi kuhusu Afrika mjini Dar es Salaam ambapo rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na waziri mkuu wake Morgan Tsvangirai wametoa wito kwa jumuiya kimataifa kuondokana na mtazamo hasi kwa nchi hiyo na kuendelea kuwekeza vitega uchumi katika nchi hiyo.

        Wamesema hivi sasa nchi yao imefanya mabadiliko makubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi baada ya kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

        Viongozi hao wametoa kauli hiyo katika mdahalo kuhusu Zimbabwe kama ina nafasi za uwekezaji au la katika mkutano huo wa biashara unaofanyika mjini Dar es Salaam.

Advertisements