PEMBA:

Huduma ya umeme mpya wa grid ya taifa kutoka Tanga hadi Pemba unatarajiwa kufanyiwa majaribio kiswani humo wakati wowote kuanzia kesho.

 Kwa Mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Kisiwani Pemba, zinadai umeme huo utafanyiwa majaribio baada ya kuwepo ahadi ya mradi wa umeme huo unaofadhiliwa na serikali ya Norway utamalizika mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo meneja wa shirika la umeme Pemba Salum Masoud hakuwaza kupatikana kuzungumzia majaribio hayo kutokana na mawasiliano yaliofanywa na mwandishi wetu kwa njia ya simu kuwa mabaya.

Hivi karibuni rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume akizungumza katika siku ya wafanyakazi duniani Mey mosi amesema mradi wa umeme kutoka Tanga hadi Pemba umo katika hatua za mwisho za kukamilika.

        Kisiwa cha Pemba kwa muda mrefu hakina huduma ya umeme wa uhakika kutokana na vinu vya kuzalisha umeme kuwa vibovu.

 Kuwepo kwa huduma hiyo ya grid ya taifa kutoka Tanga kutachochea maendeleo ya kisiwa hicho hasa katika uwekezaji wa sekta ya utalii.

Advertisements