WILAYA YA KATI:

        Wakulima wa kilimo cha umwagiliaji maji wa vijiji vya Mchangani na Tunduni Wilaya ya kati wameiomba wizara ya kilimo mifugo na mazingira na taasisi nyingine kusaidia mradi huo ili kukuza maendeleo ya kilimo.

        Katibu wa wakulima hao amesema michango mbali mbali inahitajika kuendeleza mradi huo wa kilimo ikiwemo kifedha ili kuziba pengo la kiasi cha Shiling Milioni 30 ambazo zinahitajika kukamilisha kilimo hicho.

        Aidha amesema ili kilimo hicho kiwe cha kisasa kunahitajika Matrekta yenye uwezo ili kujitosheleza kwa chakula na kupambana na Umasikini        Akizindua mradi huo waziri naeshughulikia Muungano na Mbunge wa jimbo la Uzini Mohammed Seif Khatib amewataka wakulima hao kutunza mradi huo ili kutoa nafasi kwa wengine kupatiwa msaada wa kuanzisha mradi kama huo

        Mradio wa kilimo cha Mpunga wa umwagiliaji maji unaolimwa katika vijiji hivyo ni matokeo ya ushirikiano kati ya serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya muungano chini ya ufadhili wa TASSAF

Advertisements