TANGA:

Watoto wenye ulemavu wa ngozi Albino wanaosoma katika skuli ya msingi ya Pongwe mjini Tanga wamemuomba rais Kikwete aidhinishe hukumu ya vifo ikiwemo kunyongwa hadi kufa zinazotolewa na mahakama kwa watu wanaopatikana na mauwaji ya albino.

Wamesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatia hofu watu wanaohusika na mauwaji hayo na hatimae kutokomeza vitendo hivyo vya mauwaji dhihi ya albino.

Mbunge wa kuteuliwa Atheman Kugiri amesema mauwaji ya Albino yamekuwa yakiendelea kutokana na kuwepo kwa mtandao mkubwa ambao haujaweza kufahamika.

10

Advertisements