ZANZIBAR: Chama cha Demokrasia makini kimesema kinatarajia kushinda baadhi ya majimbo ya Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na chama hicho kujimarisha marisha vizuri katika katika uchaguzi ujao. Akizungumza na wandishi wa habari makamo mwenyeki wa chama hicho Tabu Mussa Juma amesema chama hicho kimejimarisha zaidi katika majimbo ya Unguja na Pemba na kwamba kina matarajio ya kushinda. Akizungumzia ratiba ya uchaguzi wa chama hicho amesema fomu za wagombea udiwani, uwakilishi na wabunge zitanza kutolewa tarehe 15 mwezi huu hadi tarehe tano Julai. Aidha Juma amesema fomu za kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kupitia chama hicho zitaanza kutoklewa mwezi ujao hadi tarehe 30. Makamo mwenyeki huyo ambapo yeye mwenye ametangaza kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia chama hicho pia ametoa wito kwa wananchama wengine kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi huo. Uchaguzi mkuu wa Zanzibar utakao wachaguwa madiwani, wawakilishi na rais wa Zanzibar unatarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu

Advertisements