DAR ES SALAAM:

        Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profis Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza nia yake ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya muungano Tanzania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.

        Profisa Lipumba ametangaza nia hiyo wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la CUF uliofanyika mjini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe 52 kati ya 61

         Aidha ameliagiza baraza hilo kuandaa sera za kisayansi kwa ajili ya uchguzi wa mwaka 2010.

        Profisa Lipumba ashagombea nafasi ya urais kwa mara ya tatu mfululizo amewataka viongozi wengine wa vyama vya siasa na kuahidi endapo atachaguliwa ataunda serikali ya umoja wa kitaifa