ZANZIBAR:

        Waziri wa nchi afisi ya waziri kiongozi Hamza Hassan Juma amesema licha ya serikali ya umoja wa kitaifa kutarajiwa kujenga umoja na mshikamano, lakini pia inaweza kuleta changamoto za kiutendaji.

        Akizungumza na redio moja nchi waziri Juma amesema serikali hiyo inaweza kujenga umoja na mshikamano wa wananchi ili kupunguza mivutano, lakini inaweza kusababisha mivutano kwa viongozi waliomo serikalini.

Amesema athari za kupambana na upinzani ndani ya serikali ni kubwa kuliko upinzani ulioko nje, hivyo amesema hali hiyo inaweza kusababisha utendaji wa serikali kusuwa suwa na kujiuzulu njiani kwa viongozi endapo kutatokea serikalini

Hata hivyo waziri Juma amesema hawezi kusema kama serikali ya umoja wa kitaifa inaweza kuwa na faida au hasara, lakini jambo la msingi nii kungalia wazanzibari wanataka

Serikali ya mapinduzi Zanzibar tayari imeshapitisha sheria ya kuitisha kura ya maoni itakayotoa ridhaa kwa wananchi juu ya kundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa au la.

Advertisements