ZANZIBAR:

Umoja wa nchi za Ulaya E.U leo unatarajia kufanya mdahalo wa wazi utakaowajumuisha zaidi ya watu 130 kutoka makundi yaliyoko katika chuo kikuu cha Zanzibar SUZA.

Mdahalo huo utayashirikisha makundi yaliyosahaulika kutoka maeneo Unguja na Pemba ili kushawishi kufanyiwa mabadiliko na taasisi za serikali, kiraia, vyombo vya habari na jamii kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine washiriki wanatarajiwa kuelezea vikwazo wanavyopambana navyo, na kupendekeza suluhisho ili kutoa mchango wao katika harakati za kupunguza umasikini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania tawi la Zanzibar TAMWA Makundi hayo ya waliosahaulika yanahusisha watu wenye ulemavu, wanawake, vijana, wafanyakazi wa majumbani na wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari.

Mdahalo huo umeandaliwa na jumuiya ya Ulaya EU kwa mashirikainao na TAMWA.

Advertisements