DAR ES SALAAM:

Manuwari ya kijeshi ya Uingereza imewasili nchini Tanzania kukabiliana na vitendo vya uharamia katika bahari ya Hindi.

Manuwari hiyo itakayoshiriki katika harakati za ulinzi chini ya majeshi  ya nchi za magharibi NATO itahusika zaidi katika vita dhidi ya maharamia katika ghuba ya Aden ukanda wa Somalia.

Akizungumza katika mapokezi ya manuwari hiyo balozi wa Uingereza nchini Tanzania amesema tatizo la uharamia limejidhihirisha kwamba halina mipaka.

Amesema tatizo hilo ni kubwa linalohitaji umoja katika kukabiliana nalo

Advertisements