Saud Arabia's Flag

DAR ES SALAAM:

Mtoto wa mfalme wa Saud Arabia Abdula Al-faisal amesema wafanya biashara nchini Saud Arabia wanaendelea na mipango ya kuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya kilimo.

Akizungumza na shirika la ungazaji Tanzania amesema wafanya biashara hao tayari wamekuja nchini mara mbili kwa ajili ya kuangalia kuanzisha mradi wa pamoja wa kilimo, biashara na chakula.

Faisal ameyataja mazao ya kilimo ambayo wamevutiwa wawekezaji kuekeza kwa miradi ya kilimo nchini ni mpunga, mahindi, ngano na mboga mboga.

Nae waziri wa nchi afisi ya rais utawala bora Sofia Simba amesema idadi kubwa yawafanyabiashara kutoka Saud Arabia wameonesha kuvutiwa na hali nzuri ya hewa pamoja na utulivu wa kisiasa.

Advertisements