Baadhi ya majaji wa mahakama ya rufaa wakiwa mbele ya mahakama kuu ya Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa gawride la heshima lililoashiria kwa majaji hao kuanza kusikiliza na kuzitolea uwamuzi kesi za rufaa zilizowasilishwa kamatika mahakama kuu ya Zanzibar

Na Mauwa Moh’d-Zanzibar

ZANZIBAR:

Mahakama kuu ya Zanzibar imefunga ushahidi wa kesi ya mauwaji ya afisa wa ubalozi mdogo wa china Hwang Hong Xing yaliyotokea Septemba 2006 huko Mazizini baada ya kuwasikiliza mashahidi 12 wa upande mashitaka.

Akitoa kauli hiyo Jaji Abraham Mwampashi anaesikiliza kesi hiyo amesema Mahkama itatoa uwamuzi wake June 16 mwaka huu iwapo watuhumiwa wanakosa la kujibu au la.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mwendesha mashitaka wa Serikali Sleiman Masoud kusema afisi ya mkurugenzi wa mashtaka imekamilisha orodha ya mashahidi wa upande wa mashtaka.

Awali mahakama kuu ilikataa kupokea silaya aina ya SMG inayotadia kutumika katika mauwaji hayo kama kilelezo cha ushahidi kutokana kutokana na kuzuka utata wa kutofautiana kwa namba za silaha hiyo.

Watuhumiwa wanaohusishwa katika kesi hiyo ni Salum Abdalla mkaazi wa Baja, Hassan Abdalla wa Michenzani, Khamis Ali Abdalla wa Meli nne, Bimkubwa Saidi wa Fuoni Meli tano.

Wengine ni Faki Ali Hassan wa Dar es Salam, Miraji Mohammed wa Bububu na Abdulkadir Mohd wa Kiembesamaki wote kwa pamoja wanadaiwa kumuuwa afisa wa kibalozo Xing Septemba 11 mwaka 2006.

18

Advertisements