Bendera ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki ambazo ni Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na Uganda.

ARUSHA:

Naibu waziri kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Ali Juma Shamhuna amesema serikali itahakikisha inaongeza idadi ya mahakimu na majaji katika mahakama zake ili kulinda haki za binadamu.

Shamhuna ametoa kauli hiyo mjini Arusha wakati akifungua mkutano wa majaji na mawakili wa jumuiya ya Afrika ya mashariki na kusisitiza uwajibikaji kwa watendaji hao.

Nae rais wa majaji wa jumuiya ya Afrika ya mashariki Fredick Andago amesema katika mkutano huo wa siku mbili mawakili na majaji hao wamekubaliana kesi zote za masuala ya uchaguzi zimalizike katika kipindi cha mwaka mmoja

Advertisements