RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume anaondoka nchini leo kuelekea China kwa ziara maalum ya wiki ambapo pia , athudhuria maonyenyesho ya biashara  ya Kimataifa yatakayofanyika mjini Shanghai China.

Katika ziara yake hiyo Rais Karume anafuatana na mkewe Mama Shadya Karume pamoja na viongozi na maafisa wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Miongoni mwa viongozi hao ni Waziri wa Utalii, Biashara na Masoko Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Seif Ali Iddi na viongozi na Maafisa wengine wa serikali zote mbili.

Mara baada ya kumaliza ziara ya wiki moja ya nchini China, Rais Karume anatarajia kwenda nchini Qatar kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkutano Mkuu wa Kiuchumi Duniani (WEF) utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha.

Katika mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika kati ya Juni 30-31, Rais Karume anamwakilisha Rais wa Jamhutri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Advertisements