Eneo la kwampiga duri Maruhudi linalotaka kujengwa bandari ya kisasa ya meli ya mizigo Zanzibar

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Shirika la bandari Zanzibar limesema linahitaji zaidi ya dola za Marekani milioni 400 ili kuanza ujenzi wa bandari mpya ya meli ya mizigo katika eneo la Mpigaduri, Kinazini mjini hapa.

Mkurugenzi wa shirika hilo Mustapdha Aboud Jumbe amesema ujenzi huo ulipangwa kufanyika tokea mwaka 1999 kwa gharama za Dola za Marekani milioni 40, lakini hadi kufikia mwaka huu gharama za ujenzi huo  zimeongezeka na kufikia dola za Marekani milioni 400.

Akizungumza katika mkutano uliojadili soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi karibuni amesema shirika hilo linaendelea kutafuta wafadhili watakaoshirikiana na serikali kuanza ujenzi wa bandari hiyo.

Jumbe amefahamisha kuwa shirika la bandari bado linaendelea na wawakezaji kutoka China ambao wameonesha nia ya kutaka kushirikiana na serikali katika ujenzi wa bandari hiyo ya meli ya mizigo.

Endapo ujenzi wa bandari ya meli ya mizigo utafanikiwa Zanzibar itakuwa na bandari ya kisasa yenye kuleta ushindani mkubwa kwa bandari nyingine za mwambao wa pwani ya Afrika mashariki.

16

Advertisements