Bw. Charles Philemon | Prof. Jumanne Maghembe | Bw. Alpius Machage

RUVUMA

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Profisa Jumanne Maghembe amekiri kuwepo matatizo yanayowakumba wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu katika mfumo mpya wa internet na simu za mkononi.

Amesema serikali itaongeza muda wa wanafunzi kuomba kujiunga na vyuo hivyo baada ya tarehe 31 mwezi huu.

Hata hivyo waziri Maghembe ameutetea mfumo huo akisema ni mzuri na nafuu kwa wanafunzi.

Waziri Maghembe amesema hayo mara baada ya kuwatunuku shahada wanafunzi 17 na stashahda wanafunzi 35 katika mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha mawasiliano na teknolojia cha Mtakatifu Joseph kilichoko Songe mkonai Ruvuma

Amesema tatizo lilijitokeza ni mtandao wa internet wa tume ya vyuo vikuu kuwa na njia ndogo ambayo inashindwa kuhimili mahitaji ya wanafunzi wote wanaomba.

Hata hivyo waziri Maghembe amesema serikali itaimarisha mfumo huo katika siku zijazo ili kuwapunguzia wanafunzi gharama za kujiunga na vyuo kwa kulipa mara moja hata kama anaomba vyuo vingi

Advertisements