Na Juma Abdala-Zenji Fm

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeshauriwa kusogeza mbele upigaji wa kura ya maoni kutokana na kuchelewa kutoka elimu ya uraia inayohusu upigaji wa kura hiyo.

Akizungumza na Zenji Fm radio naibu Katibu mkuu wa chama cha NLD Rashid Ahmmed amesema muda uliosalia wa kutolewa elimu hiyo ni mdogo, hivyo ameishauri tume hiyo kuangalia uwezekano wa kusogeza mbele.

Amesema kura hiyo inayotarajiwa kufanyika  Julai 31 mwaka huu bado wananchi walio wengi hawajawa na ufahamu juu ya muundo wa serikali ya mapinduzi Zanzibar inayotaka kuridhiwa katika kura hiyo

Ahmmed amesema iwapo tume ya uchaguzi itaendelea na mipango ya kupiga kura hiyo Julai 31 mwaka huu bila ya kutolewa elimu kwa wananchi chama kitakwenda mahakamani kupinga upigaji wa kura hiyo.

Kauli hiyo ya NLD imekuja huku kukiwa na madai ya baadhi ya wananchi kutofahamu upigaji wa kura hiyo na nini kinachotakiwa kukipigia kura kutoka na kukosa elimu ya uraia.

Advertisements