Jengo la Baraza la Manispaa Zanzibar liliopo mtaa Malindi mjini Zanzibar

Na Juma Abdala-Zenji Fm

ZANZIBAR:

Benki ya Dunia imeahidi kulisaidia baraza la manispaa Zanzbiar kulipatia zaidi ya dola za Marekani milioni tatu ili kuimarisha shughuli za usafi katika mji wa Zanzibar.

Waziri wa nchi afisi ya rais, tawala za mikoa na vikosi vya SMZ Suleiman Othman Nyanga amesema mradi huo utakaosimamiwa na wizara ya fedha Zanzbiar utekelezaji wake utaanza mwaka 2011.

Waziri wa nchi afisi ya rais, tawala za mikoa na vikosi vya SMZ Suleiman Othman Nyanga

Akijibu suala katika baraza la wawakilishi Nyanga amesema kwa sasa baraza la Manispaa halina uwezo wa kusafisha taka zotke za mji wa Zanzibar kutokana na ukosefu wa vifaa…

Hata hivyo waziri Nyanga amesema endapo msaada huo utakosekana serikali ya mapinduzi Zanzibar italinunulia vifaa vya kisasa baraza hilo ili kukabiliana na shughuli za usafi na uzowaji wa taka.

Hivi karibuni Baraza la manispaa Zanzibar limesema linampango wa kuzitumia taka za majumbani kama mali ghafi ya kutengenezea mbolea na kuzalisha nishati ya umeme.

Mkurugenzi wa baraza hilo Rashid Ali Juma amesema tayari kampuni moja kutoka China imeonyesha nia ya kuwekeza katika utengenezaji wa mbole na nishati ya umeme kwa kutumia taka za majumbani.

Advertisements