watoto wakitumikishwa katika ajira mbaya ambazo husababisha kutoroka skuli

Na Juma Abdala-Zenji Fm Radio

ZANZIBAR

Zanzibar ikiungana na nchi nyingine katika kupinga ajira za watoto duniani hapo kesho, bado baadhi ya watoto nchini wanaendelea kutumikishwa katika sekta za uvuvi, usafiri, utalii, majumbani,biashara ndogo na kilimo.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya tatizo la ajira kwa watoto afisa kutoka wizara ya wanawake na watoto Ameir Haji amesema idadi kubwa ya watoto hao wanatumikishwa na wazazi wao.

Amesema serikali kwa kushirikiana na shirika la kazi duniani imeweka mikakati ya kutokomeza kabisa ajira za watoto ambazo zinawakosesha kuhudhuria masomo yao ya darasani.

Ameir amefahamisha katika mkakati huo kumeundwa kamati maalum ambayo pamoja na mambo mengine imepewa jukumu la kurekebisha sheria na kuunda kitengo kitakachokabiliana na tatizo la ajira za watoto nchini

Wakati huo huo kaimu waziri wa afya na ustawi wa jamii Sultan Mohammed Mugheir amesema serikali imeandaa mikakati ya kutokomeza kabisa tatizo la ajira kwa watoto ifikapo mwaka 2015.

Siku ya kupiga vita ajira za watoto duniani huadhimishwa kila ifikapo June 12 ya kila mwaka.                                17

Advertisements