Bendera ya chama cha Mapinduzi CCM

Chama cha mapinduzi CCM bado hakijapata mwanachama mwanamke aliejitokeza kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar, huku kukiwa na idadi kubwa ya wanacha wanaume walijitokeza kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu.

Tokea CCM kutanagaza ratiba ya kutoa fomu kwa wananachama wanaotaka kugombea nafasi hiyo terehe 21 mwezi huu hadi sasa wanachama kumi na moja wameshajitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ambao wote ni wanaume.

Leo wanachama watatu wamechukua fomu za kukiomba chama chao kuwateuwa kugombea nafasi hiyo huko katika afisi kuu ya CCM Kisiwandui.

Waliojitokeza kuchukufa fomu hizo ni mfanyabiashara maarufu Mohammed Raza, waziri wa elimu na mafunzo ya amali Haroun Ali Suleiman na Mwanadiplomasia Mohammed Yussuf Mshamba.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wagombea hao wameahidi kuwatumikia wananchi wa Zanzbiar kwa kuimarisha sekta za uchumi na ustawi wa jamii.

…..2..ZANZBIAR….

ZANZIBAR……2…

Mfanyabiashara Mohammed Raza amesema endapo atachaguliwa kuiongoza Zanzibar atadumisha maridhiano ya kisisa yaliofikiwa hivi karibuni ambayo yametoa mwelekeo wa kudumisha umoja na mshikamano

Nae waziri Haroun ameahidi kuendeleza mafanikio yaliofikiwa na rais Karume, huku mwanadipolomasia Mohammed Yussuf akisema serikali yake haitakuwa ya kifahari ili kuona mapato yanatumika katika maendeleo ya wananchi.

Hadi kufikia sasa jumla ya wanachama kumi na moja wamejitokeza kuchukua fomu za kuwanaia urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi.

Wagombea waliojitokeza kuchukua fomu kuanzia tarehe 21 mwezi huu hadi jana ni makamo wa rais Dr. Ali Mohammed Shein, waziri kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, waziri kiongozi wa zamani Dr. Mohammed Gharib Bilal.

Wengine ni naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna, naibu waziri Afrika mashariki Mohammed Aboud, balozi Ali Karume, kamishna msaatafu wa michezo Bakar Hamad Mshindo na mbunge wa Chumbuni Omara Sheha.                                       30

Advertisements