Archive for July, 2010

MATOKEO YA KURA YA MAONI YAANZA KUTOLEWA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeanza kutangaza baadhi ya matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa jana ili kutoa ridhaa kwa wananchi kukubali au kukataa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo kwa wandishi wa habari mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema jimbo la Bububu kura za ndio ni 4,978, hapana 1,622 na kura zilizoharibika 141.

Jimbo la Mwanakwerekwe kura za ndio ni 3,017, hapana 2,174 na zilizoharibika 127, jimbo la Kiembesamaki kura za ndio ni 1,668 na hapana 1,086 na zilizoharibika ni 56.

Jimbo la Dole kura za ndio ni 2,429 hapana 2,527 na zilizoharibika 145 na jimbo la Kikwajuni kura za ndio 3,326 na kura za hapana ni 2,131 na zilizoharibika 92….

Matokeo ambayo bado hayajathibitishwa na tume ya uchaguzi na kubandikwa katika vituo vya kuhesabia kura jimbo la Bumbwini kura za ndio 2,464 kura za hapana 1,864 na kura zilizoharibika ni 186.

Jimbo la Kitope kura za ndio ni 1,843 kura za hapana 2,738 na kura zilizoharibika 142 na jimbo la Donge kura za ndio ni 1,226, kura za hapana 3,234 na zilizoharibika 115.

Kazi za kuhesabu kura ya maoni zinaendelea katika vutuo vingine vya Unguja na Pemba ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa tena leo katika kituo kikuu cha hoteli ya Bwawani mjini hapa.

Kura hiyo ya maoni imeripotiwa kufanyika kwa amani na utulivu huku jumla ya wapiga kura laki nne, elfu saba 950 wameandikishwa kupiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Iwapo kura za ndio zitafika asilimia 51 baraza la wawakilishi litakutana kwa mara ya mwisho Agost tisa mwaka huu kabla ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ili kufanya marekebisho ya katiba ya Zanzibar.

ZANZIBAR YAPIGA KURA YA MAONI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akitumbukiza kura yake,katika kituo cha kupigia kura ya Maoni, ya kuwezesha Uundwaji Serikali ya Kitaifa ya Zanzibar,katika Skuli ya Msingi ya Kiembesamaki Wilaya Magharibi jana,Uundwaji wa Serikali hiyo ya Kitaifa ni baada ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Octoba mwaka 2010.

Zanzibar imepiga kura ya maoni kwa amani na utulivu, huku kukiwa na idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura hiyo itakayotoa ridhaa ya kukubali au kupinga undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu.

Upigaji kura huo umeanza mapema leo asubuhi na kumalizika saa 10.00 jioni hii ambapo wananchi waliopiga kura wameelezea kuridhishwa na upigaji wa kura hiyo.

Mwandishi wetu alietembelea katika vituo vya manispaa ya mji wa Zanzibar amesema upigaji wa kura hiyo haukuwa na usumbufu mkubwa kama zilivyokuwa chaguzi zilizopita.

Jumla ya vituo vya kupigia kura elfu moja na 400 Unguja na Pemba vimetumika kupigia kura hiyo, huku baadhi ya vituo vimeripotiwa kutokea matatizo ya majina ya wapiga kura kujitokeza mara mbili, hata hivyo wananchi hao walipiga kura.

Hata hivyo mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar Salum Kassim amesema bado hajapokea taarifa yoyote ya matatizo katika vituo vya kupigia kura.

Amesema idadi kubwa ya wananchi wamejitokeza kupiga kura hiyo na kufikia zaidi ya asilimia 90 ambapo matokeo yatatangazwa ndani ya saa 26

Nae mwandishi  wetu alioko Kisiwani Pemba amesema kazi za upigaji kura katika kisiwa hicho zilifanyika kwa amani na utulivu, licha kuwepo kwa baadhi ya watu ya kuendesha kampeni za siri wakati wa upigaji kura.

Hata hivyo msimamizi wa kura ya maoni katika skuli ya Madungu Ali Mussa Said amesema……CLIPS….(SAVED-PEMBA)

Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume alipiga kura katika kituo cha Kiembe samaki na kueleza kuwa amefarijika kuona zoezi hilo linakwenda kwa amani na utulivu na kuwataka wananchi kudumisha utulivu wakati wote wa upigaji kura na baada ya kupiga kura na baada ya matokeo.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya kuweka kura ya maoni kura zote zitahesabiwa katika vituo na kutangazwa kabla ya kufanyika majumuisho ya mwisho.

Naye katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad alipiga kura yake katika kituo cha Mtoni wakati mgombea mwenza wa urais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal alipiga kura katika kituo cha Kiembe samaki.

Maalim Seif alisema kwamba kura hiyo ya maoni imefanyika katika mazingira ya amani na utulivu kutokana na maridhiano yaliofikiwa kati yake na rais Karume huku huku akisisitiza kudumishwa amani iliyopo.

Alisema ni jambo la faraja kuona wananchi wanatekeleza haki yao ya kikatiba bila ya kusukumana tofauti na miaka ya nyuma na kuwataka wananchi kuendelea kudumisha hali ya maelewano hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi huu mkuu.

Jumla ya wapiga kura laki nne, elfu saba 950 wameandikishwa kupiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Iwapo kura za ndio zitafika asilimia 51 baraza la wawakilishi litakutana kwa mara ya mwisho Agost tisa mwaka huu kabla ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ili kufanya marekebisho ya katiba ya Zanzibar.

ZANZIBAR KUPIGA KURA YA MAONI

Wananchi wa Zanzibar July 31 2010 wanatarajiwa kuandika historia mpya ya nchi yao ya kupiga kura ya maoni itakayoamua undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa au la.

Huku ikiwa imebakia siku moja bado kuna mvutano miongoni mwa wanachama wa CCM na viongozi wao, licha ya viongozi wa juu kunadi mapendekezo ya chama hicho ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Makamo mwenyekiti wa CCM rais Amani Abeid Karume amesema chama hicho kimeridhia mapendekezo hayo.

Amesema kwa mujibu wa mapendekezo hayo yanawataka viongozi wa juu wa CCM kuwahamasisha wanachama kupiga kura ya ndio ili kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa hali inayonekana kuwepo na mgawanyiko wa siri.

Hata hivyo amesema bado wapo baadhi ya viongozi hao wanaopinga mapendekezo hayo kwa kuwashawishi wananchi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa

Iwapo wananchi wa Zanzibar watakubali kutia kura ya ndio kwa asilimia 51 baraza la wawakilishi Zanzibar litakutana kwa mara ya mwisho mwezi ujao ili kuifanyia marekebidho katiba ya Zanzibar.

CCM YAWASUBIRI WAGOMBEA WAKE WATOA RUSHWA

Makamo mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Piuce Msekwa

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kitatumia kanuni zake za kuwaadhibu wanachama wake watakaothibitika kutumia rushwa katika kuomba uongozi.

Makamo mwenyeki wa CCM Tanzania bara Piuce Msekwa akizungumza na BBC amesema iwapo wanachama hao watathibitika kufanya hivyo hawatateuliwa kugombea nafasi hizo.

Amesema licha ya wanachama hao kutajwa na kubainika kutenda vitendo vya rushwa, lakini makosa hayo ni ya jinai na yanahitaji kuchunguzwa ili wachukuliwe hatua za kinidhamu za chama hicho……

Hivi karibuni baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani Tanzania bara wanatuhumiwa na taasisi ya kupambana na rushwa Tanzania TAKUKURU kwa tuhuma za kutoa rushwa ili kuchagulia katika kura za maoni kupitia CCM.

RAIS KARUME AMFUKUZA KAZI MKUU WA WILAYA YA KATI UNGUJA

Rais wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amefuta kazi mkuu wa wilaya kati Ali Hassan Khamis.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini rais Karume amefuta kazi kiongozi huyo kuanzia jana.

Taarifa hiyo imesema rais Karume amemfuta kazi kiongozi huyo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kifungu 53.

Kabla ya kuhamishiwa wilaya ya kati Khamis alikuwa mkuu wa wilaya ya mjini.

Hivi karibuni kiongozi huyo ameripotiwa kutoa maneno machafu dhidi ya serikali akidai Zanzibari imeuzwa kwa kile anachodai kupinga serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar

KARUME KUZINDUA MAJENERETA YA UMEME WA HAKIBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume amewataka wananchi kuzitumia fursa ziliopo kwa kuwekeza miradi ya kiuchumi ili kuondokana na umasikini.

Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kama vile ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, umeme na huduma za bandari na uwanja wa ndege kama njia moja wapo ya kusogeza maendeleo.

Rais Karume amesema hayo alipokuwa akizundua mradi wa majenerata 32 ya umeme wa dharura huko kituo cha Umeme Mtoni wilaya ya Magharibi.

Majenerata hayo 32 yenye uwezo wa kuzalisha umeme mega 25 yamegharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 13 ikiwa ni msaada kutoka nchi ya Norway, Uingereza na Sweeden na serikali ya Mapinduzi Zanzbiar imechangia dola milioni moja na nusu.

Kuwepo kwa majenerata hayo kutasaidia kupatikana huduma ya umeme wakati inapotokea hitlafu katika gridi ya taifa.

Matumizi ya huduma ya umeme Zanzibar yameongezeka kutoka megawati 25 mwaka 2000 hadi megawati 50 kwa Unguja na Pemba ambapo shirika la umeme Zanzibar linalipia zaidi ya shilingi milioni 500 na kuskusanya shilingi bilioni tatu kila mwezi.

WAZIRI MANSOUR NA RAIS AMANI WALAANI VIONGOZI WA CCM WANAKATAA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR

Waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid

Waziri wa maji, ujenzi, nishati na ardhi Mansour Yussuf Himid ameanza kuwalaumu viongozi wa chama cha CCM wanaochochea wananchi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia vibaya malengo ya chama cha Afro Shirazi kwa kuwagawa wananchi kwa nia ya kuleta vurugu na kuhasimiana hasa wakati wa uchaguzi.

Akizungumza katika uzinduzi wa majenerata ya umeme wa hakiba huko Mtoni Himid amesema viongozi hao wanaochochea wananchi kufanya vurugu wanako kwa kukimbilia na kuwataka wanzanibari kuepukana na uchochezi huo.

Amesema historia ya Afro Shirazi italindwa na wazalendo wenyewe wenye uchungu wa nchi yao na kuwataka wanachi kuachana na viongozi wa aina hiyo wenye lengo la kuwagawa.

……2…ZANZIBAR……..

ZANZIBAR…2

Hivyo Himid ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Agust 31 mwaka huu kwa kutia kura ya ndio.

Amesema maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa Zanzibar yamesababisha washirika wa maendeleo kuongeza misada yao katika ujenzi wa miradi ya maendeleo na kiuchumi kwa Zanzibar ikiwemo usambazaji wa huduma ya umeme.

Nae rais wa Zanzibar akizungumza katika uzinduzi huo amesema viongozi wanaowashawishi wananchi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa hawana sifa za kuwa rais wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.