Baadhi ya wafanyabiashara wakitoa mali zao katika duka lililoungua moto katika eneo la mtaa wa Vikokotoni mjini Zanzibar

Milango sita ya maduka inayomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM katika eneo la Vikokotoni imeungua moto na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Milango hiyo iliyokodishwa kwa wafanyabiashara mbali mbali ilingua moto baada ya duka moja lililokuwa likifanyiwa matengenezo ya mlango kwa kuchomwa woding ambapo chechea zake zilisababisha moto huo.

Mmoja wa wafanyabisha wa eneo hilo waliopata maafa alijejitambulisha kwa Jina la Salum amesema baadhi ya mali ziliokuwepo katika maduka hayo ziliwahi kuokolewa na nyingine kuteketea kwa moto……..CLIP(SAVE-MOTO).

Moto huo umetokea leo majira ya saa tano asubuhi, lakini bado hasara kamili ya mali zilizoungua haijafahamika

Naibu Kamisha wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi, Zanzibar Gora Haji Gora amesema wamefanikiwa kuzima moto huo kwa wakati baada ya kupata habari za kuzuka moto huo.

Hata hivyo amewataka wafanyabishara kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuweka vifaa vya dharura vya kuzimia moto ili kuepusha athari kubwa zinazoweza kutokea

Huku tukio hilo likitoa baadhi ya vijana wameripotiwa kuiba baadhi ya bidhaa zilizokuwemo kwenye maduka hayo.

Advertisements