Wizara ya afya na ustawi wa jamii, Zanzibar imesema wagonjwa 36 wanatarajiwa kupatiwa matibabu ya uti wa mgongo, ubongo na upasuwaji kwa ushirikiano wa madaktari kutoka Uhispania na wenyeji wa Zanzibar.

Waziri wa wizara hiyo Sultan Mohammed Mugheir amesema wagonjwa watakaonufaika na matibabu hayo ni wenye maradhi ya mifupa, viungo, vichwa maji, uvimbe wa ubungo na uti wa mgongo.

Akizungumza na madaktari bingwa kutoka Uhispania amesema matibabu hayo yatapunguza gharama za serikali kutoa fedha kuwasafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu.

Kiongozi wa madaktari hao amesema ujumbe huo umekuja na madaktari wenye uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa vya matibabu vikiwemo Citi Scan, X-ray na huduma za wagonjwa mahututi.

Hii ni mara ya sita kwa madaktari kutoka Uhispania kuja Zanzbiar kuwafanyia matibabu wanachi ambapo jumla ya wagonjwa 104 wameshafanyiwa matibabu chini ya mpango huo

Advertisements