Makamo mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Piuce Msekwa

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kitatumia kanuni zake za kuwaadhibu wanachama wake watakaothibitika kutumia rushwa katika kuomba uongozi.

Makamo mwenyeki wa CCM Tanzania bara Piuce Msekwa akizungumza na BBC amesema iwapo wanachama hao watathibitika kufanya hivyo hawatateuliwa kugombea nafasi hizo.

Amesema licha ya wanachama hao kutajwa na kubainika kutenda vitendo vya rushwa, lakini makosa hayo ni ya jinai na yanahitaji kuchunguzwa ili wachukuliwe hatua za kinidhamu za chama hicho……

Hivi karibuni baadhi ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani Tanzania bara wanatuhumiwa na taasisi ya kupambana na rushwa Tanzania TAKUKURU kwa tuhuma za kutoa rushwa ili kuchagulia katika kura za maoni kupitia CCM.