Wananchi wa Zanzibar July 31 2010 wanatarajiwa kuandika historia mpya ya nchi yao ya kupiga kura ya maoni itakayoamua undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa au la.

Huku ikiwa imebakia siku moja bado kuna mvutano miongoni mwa wanachama wa CCM na viongozi wao, licha ya viongozi wa juu kunadi mapendekezo ya chama hicho ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Makamo mwenyekiti wa CCM rais Amani Abeid Karume amesema chama hicho kimeridhia mapendekezo hayo.

Amesema kwa mujibu wa mapendekezo hayo yanawataka viongozi wa juu wa CCM kuwahamasisha wanachama kupiga kura ya ndio ili kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa hali inayonekana kuwepo na mgawanyiko wa siri.

Hata hivyo amesema bado wapo baadhi ya viongozi hao wanaopinga mapendekezo hayo kwa kuwashawishi wananchi kukataa serikali ya umoja wa kitaifa

Iwapo wananchi wa Zanzibar watakubali kutia kura ya ndio kwa asilimia 51 baraza la wawakilishi Zanzibar litakutana kwa mara ya mwisho mwezi ujao ili kuifanyia marekebidho katiba ya Zanzibar.