Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande

Tume ya uchaguzi Zanzibar imeanza kutangaza baadhi ya matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa jana ili kutoa ridhaa kwa wananchi kukubali au kukataa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa Octoba mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo kwa wandishi wa habari mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande amesema jimbo la Bububu kura za ndio ni 4,978, hapana 1,622 na kura zilizoharibika 141.

Jimbo la Mwanakwerekwe kura za ndio ni 3,017, hapana 2,174 na zilizoharibika 127, jimbo la Kiembesamaki kura za ndio ni 1,668 na hapana 1,086 na zilizoharibika ni 56.

Jimbo la Dole kura za ndio ni 2,429 hapana 2,527 na zilizoharibika 145 na jimbo la Kikwajuni kura za ndio 3,326 na kura za hapana ni 2,131 na zilizoharibika 92….

Matokeo ambayo bado hayajathibitishwa na tume ya uchaguzi na kubandikwa katika vituo vya kuhesabia kura jimbo la Bumbwini kura za ndio 2,464 kura za hapana 1,864 na kura zilizoharibika ni 186.

Jimbo la Kitope kura za ndio ni 1,843 kura za hapana 2,738 na kura zilizoharibika 142 na jimbo la Donge kura za ndio ni 1,226, kura za hapana 3,234 na zilizoharibika 115.

Kazi za kuhesabu kura ya maoni zinaendelea katika vutuo vingine vya Unguja na Pemba ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa tena leo katika kituo kikuu cha hoteli ya Bwawani mjini hapa.

Kura hiyo ya maoni imeripotiwa kufanyika kwa amani na utulivu huku jumla ya wapiga kura laki nne, elfu saba 950 wameandikishwa kupiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Iwapo kura za ndio zitafika asilimia 51 baraza la wawakilishi litakutana kwa mara ya mwisho Agost tisa mwaka huu kabla ya kumaliza muda wake wa miaka mitano ili kufanya marekebisho ya katiba ya Zanzibar.