Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazanzibari kukubaliana na matokeo ya kura ya maoni kuhusu undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Aidha amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wanachama katika kampeni za uchaguzi mkuu ujao kuendesha mikutano yao kwa usalama na utulivu kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Rais Kikwete ametoa wito huo alipokuwa akiwahutubia watanzania katika hutuba yake ya kila mwezi na kuwataka wananchi wa Zanzibar kukubaliana na matoko hayo ili kuepusha migogoro.

Advertisements